Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, February 18, 2011

Wakenya wanaonekana kuwa wanakunywa kiasi kikubwa cha pombe ikilinganishwa na nchi zote za Afrika mashariki ingawa Uganda ipo kileleni katika idadi ya wazalishaji wasio rasmi wa pombe .

Taarifa ya karibuni kabisa ya unywaji wa pombe iliyotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO na kuchapishwa na magazeti ya Kenya inabainisha kuwa takriban nusu ya wanywaji wa pombe nchini Kenya wanapendelea kunywa bia , wakati katika nchi za Uganda na jirani zao Tanzania wanapendelea zaidi pombe za kienyeji.

Takriban asilimia 90 ya wanyaji wa pombe katika maeneo ya mipaka wanapenda kunywa pombe za kuchachushwa kama vile waragi, muramba, tonto na nyinginezo zinazotengenezwa kienyeji.Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO , Dr. Ala Alwan ambaye anahusika na magonjwa ya kuambukiza na afya ya akili amesema kuwa nchi nyingi zimebaini madhara makubwa yanayotokana na matumizi ya kilevi kupindukia , hivyo kuna haja ya kuchukua hatua zaidi.Ripoti iliyoisifu Kenya kwa ulevi inabainisha kuwa takriban asilimia 17 ya wanafunzi wa kiume nchini humo na asilimia 12 ya wanafunzi wa kike walikutwa wakinywa pombe katika siku 30 za awali kabla ya kuanza rasmi kwa utafiti unaohusu unywaji wa pombe.

Hali hii pia imejitokeza katika nchi za Tanzania na Sychelles ambako asilimia 60 ya wanafunzi wa Sekondari, high schools, na vyuo vikuu wanakunwa pombe kwa viwango tofauti.Taarifa hiyo inasema kuwa mbali na imani iliyojengeka awali kuwa Wakenya si wanywaji sana wa pombe , lakini ukweli ni kuwa wale wanaokunywa , wengi wao huwapiga wake zaozaidi ya mara mbili kwa wiki, chanzo kikiwa pombe.Sijui inatupa picha gani watu wa Afrika Mashariki. Bila shaka ni kupanuka kwa soko la Kilevi na kuongezeka kwa ‘walevi’ katika eneo letu . au siyo!

0 comments: