Jana nilikuwa na mgeni katika studio za Utangazaji za Redio Japani-NHK World . Huyu ni msichana wa kijapani mwenye miaka 30 aitwaye Eriko Mukoyamamaarufu kwa jina la Anyango.
Alikuja hapo kuandaa vipindi tukishirikiana naye vinavyohusu wanamuziki wa Japani na vitatangazwa kuanzia mwezi April mwaka huu. Mwanzoni kabisa katika mahojiano yetu alijitambulisha kuwa 'Mimi ni Mjapani wa Afrika, Nimezaliwa Tokyo lakini moyo wangu wote uko Afrika', ikanigusa sana kama Mwafrika.
Binti huyu amejikita sana katika muziki wa kiasili wa kiafrika na ni mtaalamu wa kifaa cha kitamaduni cha Kijaluo kinachojulikana kama 'nyatiti' , gitaa la kiasili la nyuzi nane.
Mdada huyu anapiga kifaa hicho akiimba nyimbo za Kijaluo na kiswahili. Anasema kuwa ameweka historia kuwa mwanamke wa kwanza duniani kuruhusiwa rasmi kukipiga chombo hicho kwani kwa asili hupigwa na wanaume tu.
Ameshatoa album zake mbili mpaka sasa na wiki hii anaelekea Ufaransa kufyatua albamu zake ya tatu. Aliwahi kuishi Kenya katika harakati zake za kujifunza nyatiti katika vijiji vilivyopo magharibi ya nchi hiyo akikata kuni, kuchota maji na kusonga ugali.Bila shaka mengi yanayomuhusu unaweza kuyapata kuitia katika vipindi tulivyoviandaa.
Unaweza kumuangalia akiwa stejini anavyofanya vitu vyake...
CCM IRINGA YAMPA TUZO MAALUM MNEC SALIM ASAS
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment