Mwanamume mmoja mkazi wa Warabi mkoani Saitama, amehukumiwa kwenda jela miaka mitano juzi Ijumaa na mke wake amehukumiwa kwenda jela miaka minne na usu kufuatia kifo cha mtoto wao wa kiume kilichotokea mwaka 2008 kutokana na ugonjwa wa kwashakoo.
Wanandoa hao Masami Shindo(47), na mkewe Sanae, (37) walikabiliwa na tuhuma za kuzembea kumpa lishe mtoto wao wa kiume na mahitaji ya kitiba kuanzia mwaka 2007 mwezi desemba wakati mtoto huyo akiwa na miaka minne hadi pale alipofariki dunia mwaka 2008 kutokana na kushikwa na na ugonjwa wa “Acute encephalopathy” , kwa kiswahili ‘ enkefalopathi sugu”.
Kulingana na taarifa ya polisi mvulana huyo mdogo alikuwa na uzito wa kilo 10 wakati anapoteza maisha. Polisi wamesema kuwa Shindo alikanusha kuwa mzembe katika kumlea mtoto wao akisema kuwa alikuwa akimpa chakula vizuri. Wanandoa hao wana watoto wawili mkubwa ana miaka kumi na kutokana na vifungo walivyopata wazazi wake mtoto huyo amepelekwa kwenye kituo cha kulelea watoto hadi pale wazazi wake watakapomaliza vifungo vyao.
Hali ya utapiamlo kwa watoto ni tatizo kubwa katika nchi hasa zinazoendelea....Picha hiyo ya mama anayenyonyesha imepigwa Kambodia katika familia yenye maisha duni...mtoto anataka kunyonya, maziwa hakuna..Ila hili la japani lipo 'tofauti kidogo 'Jaji kasema.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Monday, February 28, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment