Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, February 28, 2011

Idadi ya ‘ ndoa bandia' zinazowahusisha raia wa kigeni ambazo zimefichuliwa na jeshi la Polisi kote nchini Japani kwa mwaka 2010 kuwa zilifikia 153 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Taifa la Polisi hapa Japani.

Polisi walichukua hatua malimbali ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali, kukamata na kupeleka nyaraka kwa waendesha mashitaka dhidi ya watu 471 wakihusishwa na tuhuma hizo. Shirika hilo limesema kuwa Polisi wanafuatilia miendendo ya ndoa hizo ‘bandia ‘ zenye malengo mbalimbali kama vile kutengeneza mazingira ya kufanya uhalifu.Shirika hilo limesema kuwa baadhi ya raia wa kigeni walijihusisha na vitendo vya jinai baada ya kupata hati za vya ukaazi kwa hatua yao ya kufunga ndoa za raia wajapani huku vikundi vya kihalifu vikipata fedha kutokana nandoa hizi za kupanga.

Source: http://www.japantoday.com/category/crime/view/no-of-fake-marriage-cases-involving-foreigners-surges-in-2010

0 comments: