Fally Ipupa maarufu kwa jina la Di Caprio alizaliwa katika jiji la , akiwa Kinshasa katika familia ya mzee Ipupa Ebombo na mama Bolotuli Mbo mwaka 1977.
Alianza muziki tangu akiwa mdogo akiwa anaimbia bendi mbalimbali ambazo hazina majina huko DRC lakini jina lake liliibuka kwa kasi pale alipofanikiwa kuwa muimbaji wa kutumaini wa katika bendi ya Quartin Latin chini ya mmliki wake Koffi.
Fally alikuwa muimbaji wa kofii kutoka mwaka 1999 aliweza kufanya kazi kadhaa alipokuwa katika kundi la Quartin Latin ukiwemo wimbo wa Pharmacien katika album ya Monde arabe, aliweza pia kutunga wimbo wa Ko Ko Ko katika album ya (Affaire d'etat) pamoja na Eternellement (kwenye Force de frappe). Fally anasema yeye anavutiwa sana na mashairi ya Koffi na Papa Wemba kutokana na sauti yake lakini pia JB Mpyana Mpiana na Werrasone ni miongoni mwa wanamuziki anaowapenda.
Mwanamuziki huyu ana staili yake ya kuimba muda mrefu na kuacha muziki wa vyombo vitupu kiduchu tu…lakini staili hiyo haiwachoshi wapenzi wake kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutunga mashairi Wale wanaojua kilingana hushikwa vilivyo na mashairi hayo na wale wasiojua lugha hiyo huvutiwa na mirindimo ya vyombo na sauti ya hisia kali aliyo nayo mwanamuziki huyu.
Ngoja nijaribu kukupa tafsiri ya wimbo huu subra! hii ni tafsiri yangu , pamoja na mapungufu yake unaweza kupata picha anachoisema!
Anaanza Ipupa; "Lakini tunakwenda kusubiria wapi?
Subiri….”Wako wapi sasa wale waliokuwa wakisema kuwa kitu mapenzi hakipo kabisa, Sasa hayo unaweza kuyaita nini?Kitu gani kimenipata, unaona nimekutana na wewe na moyo wangu ukatingishika!
Nimekua nikiwa mtu mwenye haya nyingi hata wazazi wangu wakitumai kuwa nitakuwa Kasisi siku moja ,wewe umeubadilisha mpango mzima wa maisha yangu,
Lepe zito la mapenzi limenizingira hadi katika nywele kichwani mwangu, unaweza kuwa na wasiwasi juu ya chochote lakini si wasiwasi juu ya mapenzi niliyonayo kwako. Mapenzi yameniweka katika hali ya kustaajabisha , kama vile kuangusha kilio bila ya kupigwa,
Chorus: Ni kwa umbali gani, mapenzi yako yamenisukumuma kwenye kaburi langu, ona nywele zangu za mvi zimeanza kurudia weusi wake tangu ulipoanza kunipenda!
Mtu anaposubiri boti huenda gatini,
Mtu anaposubiri ndege huenda Airport,
mtu anaposubiri treni huenda stesheni ya treni,
lakini pale mtu anaposubiri mapenzi anatakiwa aende wapi?
Si Ulianiambia nisubiri eti kwasababu mapenzi yanasubiwa…kweli!
…Nashangaa kama hilo bunge lililo katika moyo wako tayari limekwishaitisha mkutano kujadili suala letu , wewe Josee Mapwata…”
Hebu fuatilia mdundo na maneno ya Fally Ikupa kwa kubofya hapo!...
TAWJA :KESI ZA UBAKAJI,ULAWITI ZINAONGEZA
51 minutes ago
1 comments:
nimependa tafsiri za nyimbo za fally ipupa lakini naomba uweke pia tafsiri za nyimbo za koffi Olomide, kwa kweli wengi tunapenda hasa watu wanaonizunguka mimi.
Post a Comment