Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, March 12, 2011

Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani , Bw. Francis Mussongo ametoa wito maalum kwa watanzania wanaoishi nchini Japani kuchukua hadhari kufuatia habari za kuvuja kwa mnunurisho wa nyuklia. Hii ni taarifa yake kamili;


Ndugu watanzania mliopo Japani,
Kwa Mujibu wa taarifa zinaendelea kutolewa na NHK Japan, mitambo ya Nuclear Fukushima Plant (1) kuanzia saa 10 jioni kwa muda wa Japan inatoa radiations na kuna dalili za mlipuko katika kituo hicho, Hali hii imepelekea kutangazwa kwa hali ya dharura na watu wote wa maeneo hayo wanatangaziwa kuondoka maeneo ya karibu na eneo hilo ili kuepusha madhara endapo hali hii itaendelea. Endapo mlipuko utatokea kuna uwezekano wa kuleta madhara kwa watu na mali hadi umbali wa kilomita 10 kutoka eneo la Kinu hicho cha Nyuklia. Kwa kutambua kuwa kuna watanzania wenzetu katika eneo la Fukushima kupitia mtandao huu tunaomba wenye mawasiliano na wenzetu waliko Fukushima kuwajulisha kuondoka katika maeneo hayo. Tahadhari pia inatolewa pia maeneo ya Fukushima kuna uwezekano wa kutokea Tsunami tunashauri wenzetu waliko huko wajulishwe kuondoka maeneo ya ufukweni ili kujihami.
Francis Mossongo,
Afisa mwandamizi Ubalozi wa Tanzania,Tokyo...12, March, 2011


Wakati huo huo... ++ Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika Vilivyoitaarifu Mirindimo hivi punde watanzania wote wako salama hapa Japani...

0 comments: