Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, March 09, 2011

Tetemeko kubwa la ardhi lililo na ukubwa wa 7.2 limetikisa eneo la Kaskazini Mashariki mwa Japani muda mfupi kabla ya kugonga saa sita mchana kwa saa za Japani (Afrika Mashariki asubuhi ya saa 12) .

Shirika la utabiri wa hali ya hewa lilitoa hadhari ya kutokea mawimbi ya tsunami katika eneo hilo hususan katika pwani ya bahari Pacifiki ikiwa ni pamoja na mikoa ya Aomori, Iwate, Miyagi na Fukushima prefectures. Mawimbi ya tsunami yanatarajiwa kuwa ya kimo kinachofikia sentimeta 50 na halitarajiwi kuleta madhara makubwa.
Tetemeko hilo limetikisa hadi katikati ya jiji la Tokyo, nasi tuliokuwemo katika jengo la Shirika la Utangazaji la Japani tulilisikia likirindima , japo teknolojia ya kukabili matetemeko ilitunusru, ambayo huyafanya majengo kuwa katika hali ya kuyumba ‘Kwa kuelea’.Shirika la hali ya hewa linasema kuwa kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika rasi ya Ojika kilometa chini ardhini na mawimbi yenye kimo cha sentimeta 60 yaliripotiwa kuonekana katika bandari ya Ofunato katika mkoa wa Iwate .
Hakuna majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa na maisha yanaendelea kama kawaida. Treni ziendazo kasi zilisimama kwa muda na baadaye zikaanza safari zake za kawaida , hali ambayo pia ilizihusisha treni za mwendo wa kawaida.

0 comments: