Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, May 23, 2011

Leo katika studio za Shirika la Utangazaji -NHK tulikuwa na mwanamuziki wa kijapani Bi. Erico Mukoyama,maarufu kwa jina la Anyango ambaye hucheza chombo cha kiasili cha kijaluo kwa kuchanganya na muziki wa kisasa.

Mdada huyu aliwahi kukaa nchini Kenya na anaongea kwa ufasaha Kijaluo na Kiswahili. Alikuwa akinipa taarifa ya safari yake ya Ufaransa na maandalizi ya Albamu yake yenye nyimbo 15 na pia tulirekodi kipindi cha Sauti ya Anyango pamoja.

Anyango ni mtayarishaji mwenzangu wa kipindi hicho kinacholengwa kuwachambua wanamuziki wa Kijapani hususan ambao wana mapenzi na bara la Afrika. Unaweza kumuangalia Anyango mwenyewe akiwa mzigoni .

Kipindi cha sauti ya anyango husikika kupitia Idhaaa ya Kiswahili ya Redio Japani kila jumamosi ya wiki ya pili ya mwezi na unaweza kuvisikiliza vipindi hivi na vingine vinavyotangazwa na NHK -Swahili kwa kubofya hapa:
www3.nhk.or.jp/nhkworld/swahili au kuia kwako kuna maneno NHK WORLD Swahili ...column ya Marafiki . Bonyeza hapo utaingia kwenye ukurasa huo.
Baada ya kazi tulipiga picha ya kumbukumbu....

0 comments: