Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, June 02, 2011

Waziri Mkuu wa Japani Naoto Kan leo ameponea chupuchupu kung’olewa madarakani baada ya kura ya kutokuwa na imani na utawala wake kupigwa na matokeo yake ‘hazikutosha’. Vyama vitatu vya upinzani viliwasilisha mswada wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwenye Baraza la Chini la Bunge jana Jumatano na upigaji kura ukafanyika leo Alhamisi mchana wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza hilo.

Ni wajumbe 152 tu kati ya 480 walitaka Kan aondoke , wakati wajumbe 293 walikataa na kumfanya aendelee kubaki madarakani. Kan aliyeonekana mchovu na mwenye usingizi( Bila shaka kutokana na majukumu mengi na chagizo za namna hiyo) alikuwa akifuatilia kwa makini zoezi hilo na baada ya kutangazwa kwa matokeo alitoa salamu ya kijapani kwa kuinamisha kichwa chake na kutoka nje ya jengo hilo.

Kan ni Waziri Mkuu wa tano wa Japani tangu mwaka 2006 , aliyeingia madarakani mwezi June mwaka jana amekuwa akichagizwa aachie madaraka hata kabla ya janga la Machi 11 halijatokea. Viongozi waandamizi wa chama chaake cha DEMOCRATIC wanadai kuwa Serikali kwa kiasi kikubwa inahitaji kuwasaidia watu waliokumbwa na maafa na si wakati wa kuonyeshana ubabe wa kisiasa. Takriban wabunge 150 wa upinzani walipiga kura ya ndio mswada huo uliopendekezwa na wapinzani wa Waziri Mkuu walihitaji walau kura 82 kutoka ndani ya muungano wa vyama tawala ili kupata kura 232 zinazohitajika ili kupitisha mswada huo kwenye Baraza hilo la chini la bunge jambo lililoshindikana.
Kufuatia kuwasilisha kwa hoja hiyo, maofisa watano waandamizi wa chama tawala cha DEMOCRATIC wakiwemo Manaibu Mawaziri wameshajiuzulu. Zaidi ya wabunge 70 wa chama tawala cha Democratic waliiambia Shirika la Utangazaji la JAPANI-NHK kabla ya upigaji kura kuwa kwamba watapigia kura ya ndio mswada ho, wakati 40 wengine bado walikuwa hawajaamua msimamo wao mpaka dakika ya mwisho. Kuna maneno kya chini chini kuwa uongozi wa chama cha DEMOCRATIC unadhamiria kuwafukuza wale wote watakaopiga kura ya kuiondoa Serikali ya KAN madarakani. Kama kura ya kutokuwa na imani na Kan ingefanikiwa bila shaka angelivunja mara moja Baraza la chini la bunge na kufanya uchaguzi mkuu mpya kama ambavyo alivyokaririwa na vyombo vya habari.
Rais wa chama cha upinzani cha LIBERAL DEMOCRATIC SADAKAZU TANIZAKI na kiongozi wa chama cha KOMEI NATSUO YAMAGUCHI wamekubaliana kwamba KAN hana sifaya kuendelea kuongoza hasa linapofika suala la kujenga upya eneo la Kaskazini mashariki lililokubwa na tetemeko la ardhi na kufaulu kushughulikia janga la Mtambo wa Nishati ya Nyuklia wa FUKUSHIMA.
Chanzo: Live coverage Radio/ TV

0 comments: