Watanzania wanaoishi nchini Japani chini ya jumuia yao inayojulikana kama TANZANITE imemchagua Bw. Rashid Njenga kuw mwenyekiti wao mpya akichukua nafasi ya Dr. Simba ambaye ameachia wadhifa huo hivi karibuni. Bw. Njenga (Pichani , aliyesimama na karibu yake , Balozi wa Tanzania nchini Japani, Mh. Salome Sijaona) ni Mkurugenzi wa Brilliant Auto & General Trading Company Ltd
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu Mkuu wa TANZANITE ,Jullius L. Mwombeki Jnr mara baada ya uchaguzi huo uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania Kamiyoga., Setagaya ku Tokyo. Majina na nafasi za waliochaguliwa ni kama ifuatavyo:
1. Njenga, Rashid - Mwenyekiti
2. Sugai, Prosper - Makamu Mwenyekiti
3. Ntyangiri, Christopher - Mweka Hazina
4. Kidume, Ahmed - Mweka Hazina Msaidizi
5. Jumbe, Fresh - Mwenyekiti Kamati ya Usuluhishi/ Nidhamu
Wajumbe wengine na nafasi zao zinabakia kama zilivyokuwa awali.
Taarifa na picha zaidi bofya; www.mumyhery-jp.blogspot.com
Maagizo ya rais ni nini?
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment