Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, July 16, 2011

Hivi karibuni , mbao za matangazo katika Chuo Kikuu Cha kilimo cha Tokyo maarufu kama Tokyo NODAI hapa Japani zilikuwa zimepambwa kwa matangazo kama inavyoonekana hapo pichani.

Matangazo hayo yaliyokuwa yameandikwa kwa Kijapani na picha nzuri za wanyamapori, na bendera ya Tanzania yalitumika kuwaalika watu kuja kujumuika katika Tafrija ya kubadilishana utamaduni wa Chakula (Food Culture Exchange Party) au kwa lugha rahisi hujulikana kama 食文化 パーティ. (Mdau Eustadius Francis akiwa katika harakati..... )

Hii ilikuwa mara ya kwanza kabisa kwa nchi ya Afrika kushiriki kwenye tafrija hizi. Katika tafrija hiyo wanafunzi wajapani wengine kutoka nchi mbali mbali wanaosoma chuoni hapa walishiriki. Kabla ya mapishi kuanza kulikuwa na presentation inayoelezea Tanzania kwa Ujumla.

Kwa hiyo siku hiyo Wajapani walielekezwa namna ya kupika wali wa nazi, mchuzi wa kuku ulioungwa kwa nazi pamoja viungo vingine. Pia tuliwaekeza namna ya kutengeneza Kachumbari ya nyanya, karoti, tango, vitunguu maji na limao. Baada ya maelekezo, kila kundi lilijiweka sawa na kutengeneza msosi bomba kabisa wenye asili ya pwani.

Hali iliyomfanya kila Mtanzania aliyekuwepo hapo kujihisi yupo nyumbani. Baada ya tafrija, waandaji waliahidi kuwa siku nyingine watapiga ugali.

Jitihada za kupata unga kutoka makampuni ya nyumbani tanzania zinaendelea ili ugali uweze kutinga katika Mesi za Chuo hicho hivi karibuni. Thanx mdau Eustadius Francis ...

0 comments: