Hivi karibuni (1/8-8/8) kulikuwa na maonyesho ya kilimo ya nane nane katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Kwa kanda ya Mashariki yalifanyika mjini Morogoro. Kulikuwa na pilika pilika nyingi uwanjani , mabanda yalikuwa mengi , wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo walijitokeza kwa wingi na raia wa kawaida kama mimi pia tulijitokeza. Kiingilio kilikuwa shilingi elfu moja kwa mtu mmoja. Nilihudhuria kwa siku mbili mfululizo. Nilishuhudia magari mengi yakibaki nje. Nilipouliza kulikoni, waliniambia safari hii viwango vya ada ya magari vilikuwa vikubwa sana. Siku moja kuingiza gari ilikuwa elfu 35 , ingawa kwa wiki ni elfu 50. Nilipata hisia kuwa pesa nyingi ziliachwa nje ya geti…
Mama ntilie nao walikosa biashara , bila shaka mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ulichangia. Lakini msisimko ulibaki ule ule wa miaka yote, hakuna jipya sana. Wakulima wadogo walikodoa tu macho kwenye mashamba ya mfano, lakini walio wengi kilimo chao wanasema hakijabadilika. Lakini ukweli unabaki palepale , kuwa na ujuzi hata kama haujatumika ni hatua kubwa. Nabakia miongoni mwa waliofika ‘8-8’ morogoro mwaka huu.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Wednesday, August 24, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment