Hivi unawajua watu 10 ambao wametambuliwa mwaka huu kuwa wana akili sana duniani na rekodi zao zimesambazwa kwenye mitandao yenye majina makubwa ulimwenguni. Hapa nitakutajia wawilikati yao...
1. Kim Ung-Yong: huyu anaishi Korea , si tajiri sana duniani. Aliingia Chuo Kikuu akiwa na miaka minne na kumaliza shahada yake ya udaktari akiwa na miaka 15 . Inaelezwa kuwa anakiwango cha juu kabisa cha akili duniani kinachojulikana kitaalamu kama IQ scale.
2. Akrit JaswalYeye ni daktari mpasuaji na umri wake ni miaka saba tu. Huyu ni mhindi na IQ yake imefikia kiwango cha f 146. Alikuwa daktari wa upasuaji pale alipomtibu mgonjwa wa kwanza, msichana aliyekuwa na miaka 7 ambaye alikuwa masikini na aliyekuwa hana fedha za kwenda kumuona daktari. Kwasasa anasomea masuala ya mahesabu katika Chuo Kikuu cha Chandigurh nchini India..
Cha kujua hapa ni kuwa baadhi ya watu wamezaliwa kuwa wenye akili lakini si wazuri sana yanapokuja suala la darasani. Kwa lugha nyingine unaweza kumpata mtu asiye na vyeti vingi vya darasani lakini ikifikia suala la uwezo wake wa kiakili utagundua ni mkubwa kupita maelezo. Na watu kama hawa unaweza kuwafananisha na maprofesa. Kwa bahati mbaya ama nzuri wenzetu wazungu ndio wanaweka kumbukumbu baada ya kufanya tafiti zao na ndio maana wanakuwa wao tu. Naamini waafrika nasi tumo humo lakini hatujulikani. Basi tuangalie kumbukumbu zilizopo…
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Wednesday, September 07, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment