Mwanamuziki kasaloo Kyanga aliyefariki usiku wa kuamkia Ijumaa tarehe tisa mwezi huu wa tisa amezikwa jijini Dar es salaam jioni hii.
Kasaloo katika hospitali ya Mwanayamala, jijini Dar es Salaam, ambako alilazwa tangu Jumatano iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kifua.
Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala ukisubiri mazishi ambayo yamefanyika hii leo katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.
Enzi za uhai wake Gwiji huyu alipitia bendi mbali mbali kubwa nchini ikiwemo Matimila, Tomatoma, Tancut Almasi, Marquiz original, Sambulumaa, Ngorongoro heroes na mpaka alifanikiwa kumiliki kundi lake aliloliita karubandika jazz band lililoasisiwa kule mombasa nchini Kenya mpaka likahamishia makazi yake hapa tena jijini Dar es Salaam.
Unaweza kupata kionjo cha Maquiz ya wakati huo..
Mokili...
Marehemu ameacha mke na watoto.Hadi wakati anafariki Kasaloo alikuwa akiitumikia bendi ya Sandton yenye maskani yake Manzese, jijini Dar es Salaam. Wakati wote huo alikuwa akihama na ndugu yake Kyanga songa ambaye naye alikwishafariki dunia. Moja ya nyimbo ninazozipenda sana za Hayati kasaloo Kyanga...ni huu Ninakwenda safarii....
Nakumbuka tulipokutana Nairobi, Kenya wakati fulani nikamuomba mara mbili kuniimba wimbo huo Jukwaani ...na akauimba ...Ninakwenda safari..Mwanzo
Ninakwenda safari, safari yenyewe ya masafa marefu
Najua hapa unabaki watasema mengi, pia wabaya wetu mama watafurahi
Lakini usisikie yao mama watoto
Nakwenda kutafuta maisha ya watoto wetu mama
Nitarudi kwa mapenzi ya Mungu
Tutaonana kwa mapenzi ya Mungu
(Chorus)
iyeye o mama iyeye
Safari sio kifo mama watoto
Subiri nitarudi mpenzi ee
[Mmoja wao]
Nikirudi mama nitakuletea zawadi
Nikirudi mama unipokee kwa mikono miwili ee
(Chorus Repeat)
Rudi mwanzo
Maagizo ya rais ni nini?
2 hours ago
0 comments:
Post a Comment