Mtangazaji Maarufu wa RTD, (sasa TBC), ABISAY STEVEN, amefariki dunia asubuhi ya Jumamosi (10/09). Alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili alikolazwa kufuatia kuugua kwa muda mfupi. Alikuwa bado mwajiriwa wa TBC. Nimehuzunishwa sana na kifo chake.. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi ameen.
Nilikuwa karibu na marehemu kikazi , niliamini kuwa alikuwa akiniamini , naye alijua kuwa namtumaini ...najaribu kukumbuka cha kuandika ...na panapo maajaliwa nitaandika kitu kumuhusu.. Ndugu, jamaa na marafiki zake nawapeni pole sana.
Update Kutoka: www.wavuti.com
- Taarifa Kupitia TBC1 Zinasema Kuwa Marehemu Atazikwa Kijijini Kwao Hai Mkoani Kilimanjaro kesho siku Ya Jumanne Na heshima Za Mwisho Kuuaga Mwili Zitafanyika leo Siku Ya Jumatatu Saa Nne Asubuhi Nyumbani Kwake Temeke Mikoroshoni Na Baadae Kusaliwa Kanisa La KKKT Temeke Vetenari. Abysai Steven Alizaliwa Mwaka 1951 Huko Moshi Aliajiriwa Na Rtd Mwaka 1970 Kama Mtangazaji Msaidizi Daraja La Iii Alipanda Ngazi Mpaka Mauti Yalipomkuta Akiwa Ni Mtangazaji Mwandamizi Mkuu Daraja La I Marehemu Ameacha Mjane Watoto 3 Na Mjukuu mmoja.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Sunday, September 11, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Asante kwa taarifa Msulwa na Pole kwa msiba wa aliyekuwa rafiki/mfanyakazi mwenzio.
Apumzike pema Abisay Steven.
Post a Comment