Bado kazi ya kutafuta miili ya watu waliofariki dunia katika ajali ya meli MV Spice Islanders iliyokuwa ikielekea Pemba usiku wa kuamkia ijumaa iliyopita Sept, 9 inaendelea na habari za karibuni kabisa zinaeleza kuwa tayari miili ya watu 192 imepatikana huku watu 601 wameokolewa wakiwa bado hai..
Kutwa nzima ya jana viongozi mbalimbali,akiwemo Raisi Jakaya Kikwete na Raisi wa Zanzibar , Dr. Mohamed Shein , Pamoja na maelfu ya wakazi wa Unguja na Pemba walifurika huko Nungwi na viwanja vya Maisara kutambua ndugu zao.. Viwanja vya Maiisara ambako miili ya marehemu iliwekwa kwa ajili ya kutambuliwa ulifurika watu huku vilio vikitamalaki kila kona.
]
Vikosi vya jeshi la maji , JKU , KMKM , Polisi na JWTZ vilikuwa eneo la Nungwi Kaskazini ya Unguja na viwanja vya Maisara vikifanya kazi ya uokozi ambapo ushirikiano mkubwa ulionekana baina ya vikosi hivyo na wananchi kufanikisha zoezi hilo.
Visiwa vya Unguja na Pemba na maeneo mengine ya Tanzania yamekumbwa na simanzi kubwa kipindi chote hiki hasa kutokana na ukweli kuwa meli hiyo iliyoanzia safari yake Dar es salaam, mchana wa Ijumaa na baadaye kuondoka Unguja usiku wa manane siku hiyo kuelekea Pemba ilijaza watu kupita kiasi na hivyo hofu ni kuwa familia nyingi zitajikuta zina msiba ama mgonjwa. Rekodi inaonyesha kuwa ni watu 760 tu ndio waliokata tiketi Dar es salaam na Unguja.
Raisi wa Zanzibar ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia jana ambapo hakutakuwa na shughuli zozote za burudani wala mikusanyiko isiyo na uhusiano na msiba huu.
Asanteni sana wanahabari wenzangu kwa kazi nzuri ya kutupasha kinachoendelea huko, tunathaini kazi yenu...Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa subra wote waliopotelewa na ndugu zao, na awape ahueni haraka walio wagonjwa. Huu ni msiba mkubwa kwa Tanzania hususan kwa wenzetu wa Unguja na Pemba..
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Sunday, September 11, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment