Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, September 22, 2011

Polisi wamemkamata Mfanyakazi mmoja wa Shirika la Utangazaji la Japani –NHK akituhumiwa kutumia kamera aliyoificha kwenye kiatu chake kumpiga picha mwanamke mmoja bila ridhaa yake.

Polisi wametoa taarifa hiyo rasmi siku ya Jumatatu kupitia televisheni ya Asahi kuwa Daisuke Hayashi, mwenye miaka 33, alikamatwa katika duka la nguo huko Tamachi akitumia kamera yake kupiga picha blauzi ya ndani ya mwanamke mmoja mfanyakazi wa duka hilo. Kamera hiyo ilifungwa kwenye kamba za viatu vya hayashi.

Polisi walinukuliwa wakisema kuwa Hayashi alikamatwa aliwahi kukamatwa kwa kufanya kitendo kama hicho hicho siku zilizopita. Alijitetea kuwa vitendo vyake hivyo vina nia ya kujipunguzia msongo wa mawazo ambao unamkabili kila mara.

Source : Japantoday.com

0 comments: