Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, September 21, 2011

Kimbunga kikali kimefika eneo la kattikati ya Japani leo mchana na kusababisha mvua na kuleta tishio la kutokea kwa maporomo ya udongo na kufurika kwa mito. Hadi sasa kimbunga kimeshapoteza maisha ya watu watano na wengine wawili hawajulikani walipo.

Shirika la utabiri wa hali ya hewa amesema kuwa hadi kufikia leo jumatano mchana , kimbunga hicho kinachojulikana kwa jina la Roke kilikuwa kikivuma kuelekea kaskazini Magharibi kwa kasi ya kilometa 35 kwa saa katika bahari , mashariki ya mkoa wa Wakayama. Upepo mkali wenye kasi ya kilometa 100 kwa saa umeshuhudiwa katika maeneo hayo.
Kimbunga hicho kimekuwa kikivuma kuelekea upande wa Kaskazini-Mashariki na kufanya mvua inyeshe katika maeneo ya kati na mashariki ya Japani wakati wa mvchana na mvua imerekodiwa kufika kima cha millilita 400 katika maeneo ya kati ya Japani katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Huku haya yote yakitokea Shirika la Utangazaji la Japani kupoitia Idhaa zake ilikuwa ikirusha matnagazo yake moja kwa moja kuwaeleza watu kile kinachoendelea wakati huo. Nasi idhaa ya kiswahili hatukuwa nyuma!

Polisi wamesema kuwa kimbunga kimewaua watu wanne na wawili hawajulikani walipo , wakati mtu mmoja alikutwa amekufa baharini karibu na bandari , magharibi mwa Japani , wengine wawili walikutwa wamekufa katika mito katikati na magharibi mwa japani na mwingine alianguka kutoka kwenye paa la nyumba alipokuwa akirekebisha paa lililokuwa likivija.
Inaelezwa kuwa hadi kufikia leo mchana nyumba zaidi ya 900 kote nchini Japani zilikuwa zimezingirwa na maji. Maelekezo ya watu kuhama au ushauri juu ya hatua za kuchukua imetolewa kwa watu takriban 340,000 katika mikoa 15 iliyopo magharibi na eneo la kati la Japani

Wakati huo huo, Wafanyakazi waliopo katika Mtambo namba moja wa nishati ya nyuklia wa Fukushima uliopigwa na mawimbi ya tsunami kufuatia tetemeko kubwa la ardhi , mwezi Machi tarehe 11 wanafanya kazi kubwa ya kuufanya mtambo huo usipate athari inayoweza kuleta tishio kwa maisha ya watu, wakati huu tufani ikielekea upande huo.
Tufani hiyo inayojulikana kwa jina la Roke inatarajiwa kulifikia eneo hilo leo Jumatano usiku hivyo vyuma katika mabomba ya kuingiza maji kwenye mtambo huo zinaendelea na kazi ya kutoa maji yaliyochafuliwa na mionzi ya nyuklia imesimama kutokana na upepo mkali na tufani.
Hata hivyo Shirika la umeme la Tokyo-TEPCO linalousimamia mtambo huo linasema kuwa hakuna hatari ya kuvuja kwa maji yenye mionzi kutoka kwenye majengo hayo ya mitambo.
Usafiri wa treni na mabasi ulisimama uanzia saa nane mchana, hadi saa mbili usiku ulipoanza tena .
Saa tatu na nusu hali ilianza kutengamaa..

0 comments: