Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, November 05, 2011

Eid Mubarak. Nawapeni mkono wa Eid wote mliofungua ukurasa huu. Ni siku njema kwetu sote. Nawatakia mapumziko mema , afya njema na kila lililojema. Eid Mubarak! Swala ya Eid kitaifa itafanyika kesho jijini Dar es salaam .

Kwa mujibu wa Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Muhidini Mkoyongore, Swala ya Eid Kitaifa itaswaliwa katika Masjid Al Farouq iliyoko BAKWATA Makao Makuu, kuanzia saa 1.30 asubuhi ikifuatiwa na Baraza la Eid.Hii leo waislamu wa madhehebu ya Sunni walifanya ibada yao nchini humo..
Huko Makkah na Madina kwenyewe....Zaidi ya mahujaji milioni tatu, wakiwa wamevalia nguo nyeupe, wanaendelea kumiminika kwenye viwanja vya Mlima Arafat hivi sasa, ikiwa ni sehemu muhimu ya ibada yao ya Hijja. Inaripotiwa kuwepo hali ya usalama wa kiwango cha juu. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia, Mansour Al-Turki, ameliambia gazeti la Kiarabu la Asharq Al Awsat, kwamba kila kitu kinakwenda kama kilivyotegemewa, na kwamba hakuna kitisho chochote kwa usalama wa mahujaji, wala kwa nchi.

Katika miaka iliyopita, kulikuwa na matukio yanayohatarisha usalama kwenye ibada hii, hasa kutokana na msongomano mkubwa wa watu, vurugu na moto. Mwaka 1987, mahujaji wa Iran waliandamana, na kusababisha ghasia zilizomalizika kwa vifo vya watu 400. Mwaka 2006, mahujaji 346 wa mataifa tafauti walikufa, baada ya msongomano katika tukio la kurusha mawe kwenye mnara, kama ishara ya kumlaani Ibilisi.
Mlima wa Arafat ni sehemu ambapo kiongozi wa umma wa Kiislamu, Mtume Muhammad, alitoa hotuba yake ya mwisho kwa wafuasi wake, karne 14 zilizopita. Hijja ni nguzo ya tano katika Uislamu, ambayo humlazimu kila muumini mwenye uwezo kuitekeleza, angalau mara moja maishani mwake.

2 comments:

mumyhery said...

shukran na kwako pia

Anonymous said...

Asante sana Da Mumyhery, Mwenyezi Mungu akupe kila lililo jema..