Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, November 17, 2011

Rais Robert Mugabe ameisifia Hong Kong kwa kumlinda binti yake kutokana na kudhalilishwa na waandishi wa habari wa Uingereza, chombo cha habari cha taifa cha Zimbabwe kimeripoti.

Bw Mugabe alitoa kauli hiyo alipohudhuria mahafali ya binti yake Bona katika chuo kikuu cha City huko Hong Kong. Walinzi wa binti huyo, mwenye umri wa miaka 22, walishutumiwa kwa kuwadhalilisha waandishi wa habari mwaka 2009, lakini hawakushtakiwa.Mwaka huo huo, mke wake Bw Mugabe Bi Grace hakushtakiwa baada ya madai ya kumbughudhi mpiga picha Hong Kong.Maafisa walitaka kinga ya kidiplomasia katika kesi ya Bi Mugabe.

Msemaji wa chuo hicho cha City Karen Cheng aliwaambia waandishi wa habari kuwa Bw na Bi Mugabe, ambao wanamiliki nyumba Hong Kong, walihudhuria sherehe za mahafali hayo siku ya Jumanne.Alisema Bw Mugabe na familia yake walipiga picha na wahitimu wengi "kama mzazi mwengine tu wa kawaida".Alisema "baadhi walikuwa wakiwatazama" lakini wazazi wengi hawakujua ni akina nani.Bw Mugabe anatarajiwa kuelekea Beijing katika ziara yenye nia ya kuvutia uwekezaji zaidi kutoka China.

0 comments: