Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, December 13, 2011

Jumamosi ya tarehe 17 DISEMBA 2011 kutafanyika hafla kubwa nay a kupendeza katika Hoteli ya PAN PACIFIC iliyopo jijini YOKOHAMA hapa Japani kuanzia saa 11.00 JIONI HADI SAA 2.00 USIKU kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara. Ifuatayo ni taarifa kamili ya Mwenyekiti wa Jumuia ya Watanzania wanaoishi hapa JAPANI-TANZANITE Bw. Rashidi Njenga kuhusiana na hafla hiyo.
“Ndugu Watanzania wenzangu, Naomba nichukue nafasi hii kuwaarifu kuwa maandalizi ya tafrija yetu yanaelekea kukamilika. Kufikia leo idadi ya watu waliojiandikisha imefikia 94, kati ya waliojiandikisha watu 60 wamethibitisha kuhudhuria. Tumepata muitikio mzuri kwa Wajapan waliowahi kuishi Tanzania, au wenye interest na Tanzania baadhi yao watahudhuria. Tutakuwa na DJ ambaye ana vyombo maalum vya Disco na atatupigia mchanganyiko wa nyimbo nyingi kutoka BENDI mbali mbali za nyumbani. Chakula na Vinywaji vya aina vyingi vitakuwapo. Vyote vimejumuishwa kwenye mchango utakaoutoa. Mheshimiwa Balozi Mama Sijaona ndiye atakayekuwa mgeni rasmi.
STESHENI: 1. MINATOMIRAI (Minatomirai Line + Toyoko line)
2. SAKURAGICHO (Keihin Tohoku)
 TAFADHALI FIKA SAA 11.00 KAMILI (5:00pm). FIKA KWA WAKATI.
Kwa kuwa tunatakiwa kuthibitisha namba ya watakaohudhuria mapema ili watu wa hoteli wafanye maandalizi yao. Tunawaomba wote ambao wamejiandikisha kuhakikisha wanatoa michango yao kufikia JUMATANO JIONI. Tunawaomba wale ambao hawajathibitisha wafanye hivyo na kulipa michango yao. Wenzetu ambao hawajajiandikisha tunawaomba wajiandikishe na kulipa michango yao. Wanachuo/ wanafunzi Yen3,000 kila mmoja. Watu wa kawaida Yen 3,000 - 5,000 na kuendelea. Unaruhusiwa kuchanga zaidi.
Michango inaendelea kupokelewa hadi JUMATANO TAREHE 14 DISEMBA 2011. Wale wote ambao watachagua kulipia mlangoni siku ya sherehe watatakiwa kulipa Yen 9,000 au zaidi KWA MTU MMOJA – HAKUTAKUWA NA UPUNGUFU/ UNAFUU. Ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza tunaomba kila mmoja ajiandikishe, atoe mchango wake kabla au kufikia mstari-mfu. Mlangoni kutakuwa na walinzi ambao hawatazungumza lugha nyingine zaidi ya kupokea pesa. Unaweza kubofya hapo kwa taarifa za ziada kuhusiana na mahali patakapofanyika hafla hiyo..
(http://pphy.co.jp/).

NJENGA, R MBA
Mwenyekiti, Kamati ya Maandalizi.

0 comments: