Marafiki zangu wa MIRINDIMO nawatakia kheri ya mwaka mpya. Hapa Japani tayari tumeshauanza mwaka mpya wa 2012. Jiografia imelazimisha iwe hivyo. Maeneo mengine duniani walikwisha ingia mapema kabla yetu na wengine itabidi wasubiri kwa saa kadhaa. Lakini naamini sote tutafika tu, kwa nguvu za Mungu.
Tuna wajibu wa kumshukuru Mungu kwa kufika siku hii ya leo. Wanaadamu wenzetu kwa mamilioni duniani hawakubahatika kuuona mwaka mpya, wameishia katikati au dakika moja kabla ya kugonga saa 6 usiku tayar kuingia mwaka mpya wa 2012. Wamepoteza uhai wao kwasababu nyingi , Mapenzi ya Mungu, ajali, vita, magonjwa , majanga, na wengine wameuwawa kikatili. Wametangulia. Tuliobaki na kuuona mwaka 2012, tuna wajibu wa kuanza upya leo. Tuachane na fukuto la nafsi la mwaka uliopita na tuwe na matumaini mapya . Kheri ya mwaka mpya, nawapenda nyote!
-Msulwa.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Sunday, January 01, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Nakutakia heri za Mwaka Mpya 2012!!!
Post a Comment