Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, February 13, 2012

Ndivyo ilivyotokea, ameshakufa na hawezi kurudi tena. Tumebaki na sauti na picha zake nyingi. Whitney Houston amefariki mjini Los Angeles nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 48.
Kifo kilimkuta akiwa katika hoteli ya Berverly Hilton mjini Los Angeles saa tisa na dakika 55 za mchana akiwa anajitayrasha kwa tamasha ya mkesha wa sherhe za kutolewa tunzo za Grammy. Sababu za kifo hazijajulikana mara moja lakini polisi wanasema uchunguzi unafanyika ingawa suala la madawa ya kulevya linatajwa tajwa.
Kufuatana na ukurasa wake rasmi wa tovuti inaelezwa kwamba Whitney amekua akipambana na tatizola madawa ya kulevya kwa miaka kadhaa, na alifanikiwa kuuza album, video na rikodi milioni 170 za nyimbo zake. Habari za kifo chake kimezusha wimbi mkubwa wa risala za rambi rambi katika kurasa za kijamii, kutoka mashabiki, marafiki na jamaa zake.
Whitney alisjinda tunzo mbili za Emmy na sita za Grammy pamoja na mamia ya tunzo za heshima. Anabaki kua mwanamuziki pekee kuweza kshikilia nafasi ya kwanza mara saba mfululizo katika orodha ya muziki bora 100. Alicheza katika filamu kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Bodyguard mwaka 1992 na kufanya vizuri. Kuanzia sasa tutanza kufuatilia wengine wanaomuiga Whitney kama huyu Leona lewis, msikilize...

Kwaheri W.H.

0 comments: