Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 70 ametapeliwa fedha zinazokaribia Yeni Millioni 4.5 wakati wa kuhamisha fedha kwenye benki. Polisi walisema jana Alhamisi kuwa utapeli huo ulifanywa mtu mmoja au timu ya matapeli iliyojifanya kumjumuisha mjukuu wa bibi huyo na mwakilishi wa kampuni ya kadi ya mkopo .
Mwanaume mmoja anadaiwa kumpigia simu bibi huyo mkazi wa jiji la Nagoya siku ya jumatatu saa mbili usiku akijifanya kuwa ni mjukuu wake akimwambia kuwa amebadili namba yake ya simu.
Polisi wamesema kuwa simu ya pili kwenda kwa bibi huyo ilipigwa siku ya jumanne saa 3 na nusu asubuhi ikipigwa na mtu aliyejitaja kuwa ni mwakilishi wa kampuni inayohusika na kadi za mikopo’credit Card ‘ na mtu huyo alimwambia huyo bibi kuwa mjukuu wake alikopa yeni million mbili na deni hilo linatakiwa lilipwe hadi kufikia jioni ya siku hiyo na kumtaka bibi huyo kuzungumza na mjukuu wake kupata udhibitisho juu ya suala hilo.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo aliingia mtego kwa kupiga namba ya bandia aliyopewa na matapeli siku iliyopita na mtu aliyejifanya kuwa mjukuu wake alithibitisha deni hilo na kumuomba amsaidia kwa kuhamisha kiasi hicho cha fedha kupitia kwenye eneo la maduka ya karibu kipitia mashine za fedha za ATM.
Bibi huyo alikwenda hapo na kuhamisha fedha hizo zilizofikia yeni million 4.499. Ambazo kwa fedha za kwetu ni sawa na Shillingi za kitanzania takriban Millioni 89.
Kulingana na msemaji wa Kikosi cha Polisi baada ya hatua ya mwisho ya uhamishaji fedha kukamilika , aliwasiliana na mtoto wake na ndipo alipogundua kuwa alikuwa ameingizwa mkenge kwa kuhamisha fedha kwenda kwa matapeli.
Source: http://www.japantoday.com
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, February 10, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment