Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, February 10, 2012

Eneo la kaskazini mwa Japani limeshuhudia kudondoka kwa theluji nzito hususan mwishoni mwa juma lililopita na wakati huu pia na kuleta hali ya taharuki miongoni mwa wakazi wa huko.
Vifo vilivyotokea vilivyo na uhusiano na hali hiyo ya baridi kali na theluji imefikia watu 83 hadi kufikia jana jioni siku ya alhamisi nah ii ni kwa mujibu wa Shirika linalohusika na menejimenti ya majanga ya asili na moto ya hapa Japani. Shirika hilo limesema kuwa jumla ya watu 1,184,wamepata majeraha.
Kati ya watu 83 waliofariki, 60 kati yao walifariki wakati wakiondoa theluji katika mapaa ya nyumba zao au barabarani. Theluji nzito iliyoanguka kwenye majengo na maeneo mengine yamewaua watu 15 na watu wengine wanne walikufa kwenye maporomoko ya theluji ikiwa ni pamoja na eneo maarufu la kitalii lenye chemchemi ya maji moto .
Shirika hilo la maafa limesema kuwa ajali za barabarani pia zimetokea kutokana na kuanguka kwa theluji kiasi cha kuwafanya madereva wasionane vyema wakiwa barabarani.
Hata uwanja wa ndege wa Hokkaido inabidi usafishwe ili ndege iweze kutua na kuruka(Angalia picha)
Mashirika ya Utabiri wa hali ya hewa yanatabiri kuwa theruji yenye kimo cha sentimeta 60 centimeters huenda ikaanguka katika baadhi ya maeneo ya Hokkaido katika kipindi cha saa 24 kuanzia usiku huu , siku ya Ijumaa.
Katika eneo la Sukavu , mkoani Aoomori ambako hali ya hewa imezidi kuwa baridi na kufikia hasi 12.8 leo Ijumaa zaidi ya kimo cha mita 4 za theluji zimetanda ardhini.

0 comments: