Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, February 10, 2012

Kwa miaka mingi nimekuwa nikiusikia wimbo huu lakini nilikuwa sijui maana yake leo nimeelewa na hivyo kunifanya niupende zaidi na zaidi. JB Mpyana anazungumzia ukweli wa maisha ambao una mafunzo. Hutajuta ukiusikiliza wimbo huu kisha kufuatilia maana yake. Thanks Pius Mikongoti nchini Malaysia na Shahibu Thabit kwa tafsiri.

“Kwa wasiojua lugha iliyotumika humu JB Mpiana alikuwa akiongelea mapenzi ya sasa akiwalalamikia akinadada akisema kuwa yapo wapi mapenzi ya ukweli ya enzi za mababu zetu ambapo watu walikuwa wakipendana kiukweli tofauti na siku hizi ambapo akinadada wamekuwa wakichagua wanaume kila mtu anataka mwanaume aliyesoma, mwanaume alina kazi nzuri, mwenye pesa, inakuwaje kwa wale ambao hawajasoma? Inakuwaje kwa wale ambao hawana kazi nzuri na hawana pesa?
kiujumla ameongelea mtaguso wa mapenzi wa sasa ambapo nadharia nzima ya mapenzi ni unanini? wewe ni nani? na dhana hii ndio inayojenga mapenzi kwenye ulimwengu wa sasa. Hii si tafsiri ya neno kwa neo ni majumuisho:-

L’amour est-ce aimer ou etre aimer? Bien que L’amour soit Le symbole d’un sentiment partage, etre aimer n’est jamais le signe d’un bonheur parfait = Je mapenzi ni kupenda au kupendwa? ingawa mapenzi ni ishara ya kubadilishana hisia, kupendwa kamwe si maana ya faraja iliyokamilika.
Bolingo eza maladie mabe dokotolo nango motema symptoma nango souci, kasi kisi nayango se presence ya motooyo ozali kolula, Lokola nalula masiya ye nde kisi nangai= Mapenzi ni ugonjwa mbaya, Dalili yake ni mawazo lakini dawa yake ni kuwepo kwa umpendaye,kama navyompenda Masiya(Yesu) ndio dawa yangu.

Bolingo lokola maladie contagieux tuna na bamoureux decus tuna na B’aveugles d’amour surtout na badivorces, Bakopesa yo temoignage na bango okoyoka mawa, okoyoka ngolo, okotikala stupefart, se kokamwa kamwa mama, se koimbaimba mama, se kotuna tina nzambe akela L’amour = Mapenzi kama ugonjwa wa kuambukiza lazima uwaulize waliokosa kupendwa, waulize vipofu wa mapenzi, waulize walioachika watakupa ushuhuda wao, utawaonea huruma,utakarahishwa, utastaajabika, Utakuwa unashangaashangaa mama, na kuimbaimba na kujiuliza kwa nini Mungu aliumba mapenzi.

Yango na po na nga Amida, hata na pasi tokovanda, hata bikebi tokoliya hata thomson tokotonda. Yesu kutu mwana ya nzambe babota ye na nandako ya mpata, Kasi mokili oyo ya tata naye, Likolo nase ya bango, kamweve o makamwisi mama = Kwa hiyo nimemchagua Amida katika mashaka tutaishi, hata samaki(thomson) tutakula tutashiba, Yesu ambaye ni mwana wa Mungu alizaliwa katika zizi la wanyama. Lakini dunia hii ni ya Babaye, mbingu na ardhi ni vya kwao Usishangae maajabu.

Na Kin Liboso ya kolinga moto bakoma kotuna ofandaka wapi, A biso tovandina mwalekwa nani akolinga biso mingi baboya bango na bango, Mosika eleki, bangungi baleki Taxi kutu eboya bango = Kinshasa kabla ya kumpenda mtu wamekuwa akiuliza unakoishi, Ah sisi tunaoshi Malekwa (Manzese,Uswahilini) nani atakaetupenda. Wengi wamekataliwa eti ni mbali mno mbu wamezidi huko hata Taxi haziendi huko.
Basusu liboso ya koloba Oui” bakoma kotuna otangaka wapi, Ah biso tubuka Bic mwa kala nani akolinga biso, Tika tokosa hata kokosa, Nga nazali graduet, Nga nazali licencie, Nga nazali enginieur, mpo balinga nga mama = Wengine kabla ya kusema ndio” huuliza ulikosoma wapi Ha sisi tuliovunja kalamu (Bic)yaani (kuacha shule) toka siku nyingi nani atatupenda, Wacha tudanganye mimi nina degree, mimi nina shahada ya juu, mimi mkandarasi ili tupendwe.

Basusu liboso ya kolinga moto bakoma kotuna de quele famille es-tu? Ah biso famille ezanga riche nani akolinga biso nzambe ya mpungu bandela mokili oyo otunaka mokomoko soki nani akolinga kobotama lisusu na famille ya pauvre. = Wengine kabla ya kumpenda mtu huuliza umetokea katika familia ya namna gani? Ha sisi familia fukara nani atakayetupenda,Baba Mungu rdia maumbile halafu muulize kila mtu kama yupo atayekubali kuzaliwa tena katika familia ya kimaskini.

Passe na nga eleki mabe yango naeffacer basouvernir nyoso ya mabe na bango nanga, memoir nanga eyebi kaka kombo ya Amida Chaty naye nde pelerinage edainayo petola nga mama sukolangamama, salisa nga nabika. = Maisha yangu yaliyopita ni mabaya ndio maana napenda kufufa zote mbaya kwenye ubongo wangu. Kumbukumbu yangu yajua tu jina la Amida Chaty Nimekuja kwako kama mpitaji,nitakase,nisugue nisaidie nipone.

Nalinga mindele,Bayindo,mikuse, milayi nalinga mike mpe minene, kasi chancelier wapi alatisanga palata ata bronzo hatanatolo, soit disant nga se amoureux,ancien de saio asala kala, roi de guere O mosala mpunda mama = nimependa weupe na weusi warefu na wafupi wembamba na wanene yupo wapi afisa zawadi hata medali ya chuma kifuani ieleweke kuwa mimi ni mpenzi mkongwe wa Saio( aliyepigana vita vya Saio mfalme wa vita Kazi isiyo na Mshahara……”

0 comments: