Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, February 05, 2012

Kijana mmoja wa Kijapani anayeshikilia taji la kula kwa kasi Takeru Kobayashi anaelezwa kuwa amevunja rekodi ya kula vipapatio vya kuku vipatavyo 337 katika kipindi cha nusu saa katika shindano lililofanyika huko Philadelphia nchini Marekani katika ukumbi wa Wing Bowl XX, shindano lililohudhuriwa na watu takriban elfu 20.
Kobayashi amevunja rekodi iliyowekwa mwaka uliopita na Jonathan “Super” Squibb aliyekula vipapatio 255.

Mpambano huo uliofanyika juzi ijumaa uliwashirikisha waelfu ya watu waliokuwa wakifuatilia kupitia runinga zao , ambapo hatimaye Mjep akaibuka kidedea.
Na amejinyakula takriban Dola za kimarekani Elfu 20 , kitita cha haja…

AP

1 comments:

Subi Nukta said...

Wajapani wanashinda sana mashindano haya tangu hisoria ya kuanzishwa kwake, sina takwimu ila kwa miaka mitano niliyofuatilia, hawa wanashinda sana au wanakuwa kati ya 3 bora!