Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, February 05, 2012

Bibi wa miaka 84 amenusurika kifo baada ya kufunikwa na theluji nzito kwa zaidi ya saa nne mfululizo. Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi , tukio hilo limetokea hatua chache kutoka makazi yake , eneo la Mogami , mkoa wa Yamagata hapa Japani.
Bibi huyo anayefahamika kwa jina la Kikuto Saito, aliwaambia Polisi kuwa aliondoka nyumbani kwake majira ya saa tano asubuhi siku ya Alhamisi iliyopita kukagua bustani ya nyumba yake na ndipo mapande ya barafu yaliyokuwa juu ya paa la nyumba yake ya ghorofa mbili yalipomuangukia na kumfumika na kutokana na uzito wa theluji hiyo alishindwa kujikwamua.

Polisi wamesema kuwa Sato anaishi na watoto wake wa kiume watatu ambao wakati wa tukio hilo walikuwa wametoka.
Mfanyabiashara mmoja anayefanya kazi zake kwa kuzunguka zunguka alisema kuwa jioni ya saa 10 kasoro dakika 10, anaaminika kuelezwa na jirani ya Saito kuwa bibi huyo haonekani na kulingana na habari za kipolisi jirani huyo aliingiwa na wasiwasi na ndipo walipomuona akiwa amefunikwa na mabonge ya barafu. Polisi wamesema kuwa ni uso tu ulikuwa ukionekana , jambo ambalo lilimfanya aendelee kuishi hadi alipookolewa.
Bibi huyo Bi. Saito alipelekwa hospitalini eneo la Shinsho ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akipewa matibabu ya kushindwa kupumua vyema lakini afya yake inaelezwa kuwa ni njema na kwamba anatarajiwa kutolewa hospitalini mwisho wa wiki hii.

0 comments: