Usifurahie tu mdundo ...fahamu na maneno anayosema pia... haya tuanze sasa: Ipupa anasema; "Lakini tunakwenda kusubiria wapi?
Subiri….”Wako wapi sasa wale waliokuwa wakisema kuwa kitu mapenzi hakipo kabisa, Sasa hayo unaweza kuyaita nini?Kitu gani kimenipata, unaona nimekutana na wewe na moyo wangu ukatingishika!
Nimekua nikiwa mtu mwenye haya nyingi hata wazazi wangu wakitumai kuwa nitakuwa Kasisi siku moja ,wewe umeubadilisha mpango mzima wa maisha yangu,
Lepe zito la mapenzi limenizingira hadi katika nywele kichwani mwangu, unaweza kuwa na wasiwasi juu ya chochote lakini si wasiwasi juu ya mapenzi niliyonayo kwako. Mapenzi yameniweka katika hali ya kustaajabisha , kama vile kuangusha kilio bila ya kupigwa,
Chorus: Ni kwa umbali gani, mapenzi yako yamenisukumuma kwenye kaburi langu, ona nywele zangu za mvi zimeanza kurudia weusi wake tangu ulipoanza kunipenda!
Mtu anaposubiri boti huenda gatini,
Mtu anaposubiri ndege huenda Airport,
mtu anaposubiri treni huenda stesheni ya treni,
lakini pale mtu anaposubiri mapenzi anatakiwa aende wapi?
Si Ulianiambia nisubiri eti kwasababu mapenzi yanasubiwa…kweli!
…Nashangaa kama hilo bunge lililo katika moyo wako tayari limekwishaitisha mkutano kujadili suala letu , wewe Josee Mapwata…”
du shairi limetulia..
Ni hapa...
Sekunde moja iliyopita...Mechi ya Tanzania Taifa Stars imemalizika huko Rabat na Timu ya Tanzania imefungwa kwa tabu magoli 3 kwa moja . Haabari ndiyo hiyo!
Mchezo huo ulikuwa wa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani Guinea ya Equator na Gabon. Mchezo huo ulifanyika katika kwenye Uwanja wa Marraketch. 
Stars ilikuwa katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi D baada ya kujikusanyia pointi tano, iko nyuma ya vinara Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati, zenye pointi nane kila moja na ziko katika nafasi ya kwanza na pili na kwa mechi hii Morroco inapanda kileleni. Stars ilihitaji ushindi wa angalau kuanzia bao 2-0 dhidi ya wenyeji wao Morocco,ndoto ambazo hazikutimia.
Tayari timu za Senegal, Ivory Coast, Botswana na Burkina Faso
zilikuwa zimejihakikishia tiketi ya kucheza fainali hizo za Mataifa ya Afrika, na kuziacha timu zingine zikigombea nafasi 10 zilizobaki.
Pambano hilo la Stars na Morocco lilichezeshwa na waamuzi kutoka Gabon, ambao ni Gassama Bakary, Jawo Dickory, Touray Sulayman na Camara Bakary, walioteuliwa na CAF wakati Kamishna wa Mchezo ni Zoumaro Gnofame kutoka Togo. Dakika ya mwisho kipa wa Taifa stars alifanya kazi ya ziada kuzuai michomo kuingia langoni vinginevyo yangelikuwa mengii tu. lakini vijana wamejaribu!
Leo nilikuwa mitaa ya Kawasaki hapa Japani...nilipata mwaliko maalum wa kutembelea kampuni moja ya magari inayoitwa Phenix. Kilichonivutia kwenda hapo ni kuwepo kwa Mtanzania , huyu ni Mmoja wa Mameneja wasaidizi wa mauzo, Cornel Kibona. Hatua kwa hatua...
Raisi wa Kampuni hiyo anasema kuwa wana matawi zaidi ya 20 ya kuuzia magari nchini Japani, wakiwa na akiba kubwa ya magari. Na sasa wanajiandaa kufungua matawi mengine katika nchi za Zimbabwe, Zambia na Tanzania na wanasema wanachokifanya ni kuweka bei ya chini ya magari yao hasa katika kipindi cha uzinduzi wa biashara...kazi kwako mdau ..lete oda...teh teh tehee!...du!
Marafiki tuliokutana nao Phenix..
Kibona ( Aliyepiga suti)katika majukumu-take 5 bro!:
Mwanamke mmoja nchini Japani mwenye umri wa miaka 45 anashikiliwa na Polisi kwa kumuuza binti yake kwa mteja mwanaume kwa akili ya ufanya naye mapenzi. Mwanaume huyo ana umri wa miaka 72 na ni mkazi wa eneo la Nagano hapa Japani.![]()
Taarifa zilizotolewa na polisi zimebainisha kuwa mwanamke huyo alikuwa akimchukua binti yake huyo na kumpeleka kwenye Hoteli moja jijini humo ambako alipatiwa kitita chake na kumuacha binti yake hapo aendelee na mambo yao.Inaripotiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akipokea kati ya Yeni Elfu 20 na elfu 30 kila akifanya hivyo (Sawa na shilingi za Kitanzania kati ya laki nne na laki sita ).
Ingawa umri wa binti huyo haujawekwa wazi , msichana huyo anaaminika kuwa hajafika miaka 20 na zaidi na wakati alipokutana na mzee huyo alikuwa na miaka kumi na ushee hivi…
Inaaminika kuwa watu hao walikutana kwa miaka kadhaa wakiendelea na biashara yao iliyoonekana machoni mwa watu kama ‘Uhusiano wa kifamilia’, kumbe yalikuwa mengine!
Uhalifu huo uliwekwa wazi baada ya msichana mmoja anayesoma shule moja na binti huyo kutoa taarifa polisi akisema kuwa kulikuwa na jambo lilikuwa likiendelea baina ya watu hao.Polisi wamesema kuwa mwanamke huyo alikuwa akiendelea na biashara hiyo ya kumuuza mwanawe ‘kingono ‘kwa mzee huyo kwa miaka kadhaa. Uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea
Kampuni kubwa ya komputa ya MAREKANI ya Apple imeitangaza aina mpya ya simu ya mkononi ya kisasa kabisa ya iPhone iliyo na kasi kubwa.
Iphone hiyo inawawezesha watumiaji kupakua data kwa kasi iliyo mara dufu ikilinganisha na ile ya modeli iliyotangulia. Aina hiyo ya smu ina kifaa kinachoweza kutambua sauti, ambapo watumiaji wataweza kuuliza maswali , na maswali hayo yatajibiwa kwa njia ya maandishi kwenye skrini.
Mwisho uamuzi umefikiwa....Mwili wa Profesa Wangari Maathai utachomwa kama alivyopendekeza yeye mwenyewe wakati wa uhai wake. Kamati iliyochaguliwa ili kupanga mazishi ya Wangari Maathai imesema kuwa mwili wa mwanamazingira huyo utachomwa katika maziara ya Kariokor, siku ya Jumamosi wiki hii.
Akitangaza shughuli hiyo ya mazishi, mweka hazina wa bodi ya Greenbelt Movement, Prof. Vertistine Mbaya alisema kuwa waliafikia uamuzi wa kuuchoma mwili wa mwili mujibu ya wosia aliouandika wakati wa uhai wake.
Picha inayojionyesha hapo ni kuwa uamuzi huu bila shaka unatokana na falsafa yake ya kuhifadhi mazingira!-Mhariri.




