Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, June 13, 2011

Posted by BM. on Sunday, June 12, 2011

Posted by BM. on Sunday, June 12, 2011

Maelfu ya watu wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa bingwa wa michezo ya Olimpiki mbio za marathon raia wa Kenya Sammy Wanjiru jana Jumamosi aliyefariki mwezi uliopita baada ya kuanguka kutoka kwenye ushoroba wa nyumba yake. Mazishi yalifanyika katika kijiji cha Heshima, eneo la Ol joroonok na kuongozwa na mjane wa Marehemu Trizah Njeri-pichani akiweka shada la maua.


Hata hivyo mama mzazi wa wanjiru alitinga nyumbani kwa Marehemu akiwa na panga alilolificha kwenye mfuko akidai kuwa atamkata nalo mtu yoyote anayeunga mkono mazishi hayo.
Hata hivyo mazishi yalifanyika katika uwanja wa michezo katika wilaya alikozaliwa, Nyahururu, katika jimbo la Rift Valley, huko Kenya chini ya ulinzi mkali wa polisi. Mahakama iliamuru wiki hii kuwa Wanjiru, aliyekuwa na umri wa miaka 24, anaweza kuzikwa licha ya kuwa uchunguzi unaendelea kuhusu mazingira yaliyosababisha kifo chake na kusema kuwa Wanjiru alikufa ama katika ajali, au alijiua baada ya mkewe kumfumania na mwanamke nwengine.
Mama yake Wanjiru, Hannah, alisusia mazishi hayo. Katika kile kinachoonyesha kupata heshima ya kitaifa alipigiwa saluti ya mizinga 21 wakati jeneza lake lilipoteremshwa kaburini katika shamba lake. Wanjiru alikuwa Mkenya wa kwanza kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki katika mbio za marathon za michezo ya Beijing mnamo mwaka 2008 na akihesabiwa kuwa mojawapo wa vijana chipukizi hodari.Mazishi yake yalihudhuriwa na wanariadha mashuhuri wa Kenya na watu mashuhuri.

Posted by BM. on Saturday, June 11, 2011

Mitaa ya Shibuya jijini Tokyo, dakika 5 zilizopita...

Posted by BM. on Saturday, June 11, 2011

Msichana kutoka kabila la Surma nchini Ethiopia, akiwa amejipammba vilivyo mdomoni na kubeba mabegani bunduki ya mchumba wake....yote maisha!

Posted by BM. on Saturday, June 11, 2011

Baraka obama akiwa na watoto wake Kijjini Kogelo, Kenya kabla hajainga White House. Unaweza kufikiria leo akifika hapo hekaheka zake!

Posted by BM. on Saturday, June 11, 2011

Aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani enzi za Utawala wa George W. Bush, Bi Condolezza Rice alipokutana na Kanali Qadhafi mjini Tripoli. Siasa kitu kibaya, jamaa wamembadilikia pamoja na 'iliyokuwa' tabasamu yote hiyo!

Posted by BM. on Saturday, June 11, 2011

Duh , watu bwana!..

Posted by BM. on Friday, June 10, 2011

Bofya hapo chini...

Posted by BM. on Thursday, June 09, 2011

MSHIRIKI wa shindano la Big Brother mwaka huu, kutoka Tanzania, Bhoke Egina, leo aliongea na wanahabari katika mkutano uliofanyika Hoteli katika ya Southern Sun jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo mshiriki huyo pamoja na mambo mengine alizungumzia uhusiano wake wa kimapenzi na mshiriki kutoka Uganda, Ernest Wasaki
Kwanza nikukumbushe mambo yalivyokuwa katika jumba la Big Brother then tumsikilize Bhoke mwenye...

Bhoke anasemaje ?....

Posted by BM. on Wednesday, June 08, 2011

Hawa ni wake wawili wa Kijana wa Kimasai kule nchini Kenya. Nimekutana na Mume wao na mke wa pili huyu Mjapani katika studio zetu za NHK hapa Tokyo , tumeongea mengi sana. Habari na picha zitafuata baadaye...

Posted by BM. on Wednesday, June 08, 2011

Mchezaji nyota wa Manchester United, Ryan Giggs amesababisha kuvunjika kwa ndoa ya kaka yake baada ya kugundulika alikuwa akimla uroda mke wa kaka yake kwa jumla ya miaka minane.
-Picha ;Ryan na nyingine akiwa na mkewe...Mchezaji mashuhuri wa Manchester United, Ryan Giggs ameingia kwenye kizaazaa kikubwa baada ya magazeti ya Uingereza kutoboa siri yake kuwa mbali ya kusailiti ndoa yake kwa kutembea na mrembo wa Big Brother, Imogen Thomas alikuwa pia akimla uroda mke wa kaka yake kwa miaka minane sasa.Imedaiwa kuwa Giggs alikuwa akijivinjari na mke wa kaka yake Rhodri Giggs kwa miaka minane na kuvuja kwa siri hiyo kumepelekea Rohdri kuamua kuivunja ndoa yake na mke wake.Rhodri mwenye umri wa miaka 34, alisema kuwa amehuzunishwa sana na habari za uhusiano wa kimapenzi kati ya Ryan Giggs na mkewe Natasha mwenye umri wa miaka 28. (Mrembo Imogen mwenye nguo nyeusi kwenye gari...)
"Nilikuwa na mke wangu Natasha siku ya jumamosi lakini kuanzia sasa siko naye tena", alisema Rhodri."Najua kwamba mimi na Ryan tulikuwa na migogoro wakati fulani lakini sikutegemea kama ingefikia hali hii ya kudhalilishana, nilihisi kuna kitu kinaendelea kati ya Ryan na Natasha lakini sikujua ni kitu gani", Rhodri.Gazeti la News of the World liliripoti jumapili kuwa Giggs alikuwa akilala na Natasha wakati mke wake alipokuwa mjamazito, na aliendelea kula uroda na Natasha siku moja baada ya mke wake kujifungua mtoto wa kike.Natasha inasemekana ndiye aliyeamua kuvujisha siri ya uhusiano wake na Giggs baada ya habari kuzagaa kwenye vyombo vya habari kuwa Giggs alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo aliyekuwa mshiriki wa Big Brother UK, Imogen Thomas.
"Nilipogundua kuwa alikuwa pia na uhusiano wa kimapenzi na Imogen, nilivunjika sana moyo", Natasha alitoboa siri kupitia kwa rafiki yake."Najua itaonekana ni jambo la kushangaza, mbali ya kumsaliti mkewe Stacey, alikuwa akinisaliti mimi pia kwa kutembea na Imogen", alisema mke huyo wa kaka yake Giggs.


Inasemekana Natasha na mumewe waiotalikiana walitoka siku za karibuni na kwenda kwenye mgahawa mmoja kwa chakula cha jioni na vijimaneno ndipo vilipoanza. Picha-Mgahawani-na Giggs mkubwa akiondoka nyumbani kwa huzuni akiwa amejifunika sweta asipigwe picha...Habari zaidi zimesema kuwa baada ya Natasha kuvihakikishia vyombo vya habari kuwa habari za uhusiano wake na Giggs kuwa ni za kweli, alisafiri pamoja na watoto wake wawili kwenda nje ya nchi.Rhodri kwa upande wake amebaki na majonzi nyumbani kwake ambapo inadaiwa kuwa marafiki zake wa karibu wanajaribu kumfariji kwa haya yaliyomkuta

Posted by BM. on Tuesday, June 07, 2011

Inaelezwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wajapani wenye umri wa zaidi ya miaka 35 wanaathiriwa na ugonjwa wa fizi za meno lakini hivi karibuni imegundulika kingamwili ambayo ikiwekwa mdomoni, inapambana moja kwa moja na wadudu wanaosababisha ugonjwa huo. Kingamwili hiyo imetengenezwa kwa kutokana na mayai.
Ukitaka kujua inakuwaje ... bofya hapo kulia kwenye safu wa wadau, neno NHK WORLD SWAHILI.

Posted by BM. on Tuesday, June 07, 2011




Posted by BM. on Saturday, June 04, 2011