Kuna semi nyingi za Kiswahili zilizobeba maana nzito sana. Kama vile kupanga ni kuchagua, hadhari kabla ya hatari , mtu huvuna anachopanda na kadhalika. Mustakabal wa watoto wetu mathalan hutegemea vitu vingi , kwa mfano “Majaaliwa”, matunzo na maamuzi ya wazazi au walezi , majirani , jamii na taifa. Na hatimaye kumweka katika kufanya maamuzi mazito yeye mwenyewe anapokuwa mtu mzima. Ninapoongelea jamii nina maana ya ya waalimu,wasanii, majirani , dini na kadhalika.
Jicho langu leo nalielekeza kwenye wasanii na ninaye hapa Mbilia Bel aliyejitosa naye katika malezi ya watoto kwa kutumia sauti yake. Mwanamuziki huyu ambaye hivi sasa ana miaka 50 anatoa usia katika mmoja wa wimbo wake SENDA kuwa; “Usimpeleke mwanao kwenye ndoa ya mapema , mwache asome …ndoa itamtesa”. Baadhi ya meneno katika wimbo uitwao “Senda” wa mwanamuziki Mbilia Bel. Ukiusikiliza wimbo huu utagundua kipaji cha Mbilia. Siku zote amekuwa akiitumia sauti yake vizuri inayoambatana na ujumbe mzito . Bahati mbaya wazungumzaji wa Kiswahili walio wengi hawaelewi maana ya nyimbo nyingi za Kilingala , lakini wimbo SENDA mbilia Bel ameuimba kwa Kiswahili.
Kabla ya kubofya ili kumsikiliza Mbilia Bel , hebu soma historia yake kidogo. Mbilia bel ana historia nzuri sana katika fani yake ya muziki. Alizaliwa mwaka 1959 Alianza kuimba akiwa na miaka 17 akiwa na mwanamuziki mkongwe wa zamani wa kike Abeti Masikini na baadaye akajiunga na Samangwana.
Mwaka 1981 akajiunga na mwanamuziki Tabu Ley katika bendi yake ya Afrisa International na chati yake ikapanda sana kwani mwaka 1982 alitoka na kibao chake kiichoitwa Mpeve Ya Longo,kikisimulia kisa cha mwanamke aliyetelekezwa na mumewe na kumuachia watoto awalee yeye mwenyewe , kibao kilichokuwa simulizi sana huko Zaire ya zamani sasa DRC. Mamia ya tungo na midundo ya nyimbo zote za mwanamuziki huyu zimemfanya akubalike na asichuje
Katikati ya miaka ya 80 Mbilia Bel aliona na Tabu Ley lakini baadaye wakatimuana na Mbilia bel akajiunga na Rigo star na kufyatua kibao kiitwacho Phenomene. Tabu ley naye akatumia nguvu nyingi kumuandaa Bibie Faya Tess mwanamuziki aliye kuwa chipukizi wakati huo ili kuchukua nafasi ya Mbilia lakini hakufikia kile kiwango cha Bel. SasaBofya hapo upate kile ninachokisema.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, June 06, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment