Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, September 14, 2009


Mtu mmoja ambaye alisimamisha gari lake katika eneo la kuegeshea gari kandokando ya barabara kuu moja katika jiji la Hokuto mkoa wa Yamanashi hapa nchini Japani…kwa lengo la kubadilisha tairi lake baada ya kupata pancha alikutwa na mauti baada ya gari jingine kumgonga kwa nyuma na kufariki papo hapo.Tukio hilo limetokea jana jumapili saa 10 na dakika 20. Mtu huyo ametambuliwa kwa jina la Tsutomu Yasuda na ana miaka 59 alikuwa safarini kuja hapa Tokyo. Abiria watatu na dereva wa gari iliyosababisha ajali wamejeruhiwa na Polisi wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Kwenye highways , uangalifu ni muhimu…japo ajali haina kinga

0 comments: