Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, September 15, 2009

Picha inayomuonyesha Marehemu Mohamed Mpakanjia na Mkewe ambaye pia ni Marehemu Amina Chifupa ,enzi ya uhai wao
MFANYABIASHARA maarufu na mtu mashuhuri katika fani ya michezo na Burudani nchini Tanzania Mohamed Mpakanjia amefariki dunia leo katika hospitali ya jeshi la Lugalo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana katika hospitalini hiyo ambayo pia alifia aliyekuwa mkewe Amina Chifupa, Mpakanjia amefariki dunia katika hospitali hiyo majira ya saa saba mchana jana jumatatu. Taarifa zinasema kuwa Mpakanjia alifikishwa hopitalini hapo jumamosi iliyopita kutokana na kusumbuliwa na homa ya mapafu kwa jina jingine Nimonia. Chanzo hicho kutoka hospitalini kilichokaririwa na vyombo vya habari vinggi nchini Tanzania kinasema kuwa alipofika hospitalini hapo alionekana mwenye afya njema lakini hali yake ilibadilika ghafla na mauti kumfika.
Katika uhai wake Mpakanjia alikuwa ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo na burudani hasa kutokana na kusaidia wasanii, wanamuziki na bendi nyingi za muziki hapa nchini. Alikuwa mfadhili mkuu wa bendi ya DDC Mlimani Park 'Sikinde', Tanzania One Theater 'TOT Plus' na pia alidhamini albamu za pamoja za wanamuziki Ramadhani Masanja 'Banza Stone', Ally Choki na kiongozi wa Msondo iitwayo 'Sisi ndiyo Sisi' ya mwaka 2005. Kwa upande wa sanaa alitoa mchango mkubwa kwa kuwasaidia wasanii wengi wa sanaa ya filamu na maigizo kwa kuwawezesha kifedha kukamilisha kazi zao hizo. Mungu ailaze roho yake pema peponi. Amina.

1 comments:

mumyhery said...

inna lillah wa inna ilaiyhi rajuun