Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, September 15, 2009


Nchini Afghanistan vitendo vya kuoa watoto wadogo vimetia fora na hivyo kulalamikiwa na watu wanaokataa udhalilishaji wa watoto. Pichani mzee huyo ana miaka 81 ameoa mtoto wa miaka 13 na hiyo ni siku ya harusi amepozi kupiga picha na bi harusi...du Wazazi wa watoto wa kike inasemekana huwaozesha watoto wao hata wakiwa na miaka nane kama huyu kwa watu wazima ili wapewe fedha za kujiendeshea maisha. Pamoja na vita kila kukicha lakini pia kuna vituko visivyokwisha. Kama hayo hayatoshi huko Malaysia nako kuna vituko.

Bibi mwenye umri wa miaka 107 wa nchini Malaysia ambaye alishaolewa na kuachika mara 21 amesema yuko tayari kuolewa na mwanaume mwingine kwa mara ya 23 kwasababu anahofia kuwa mume wake wa 22 anayeishi naye hivi sasa anaweza kumkimbia na kutafuta mwanamke mwingine mwenye umri mdogo.Mume wake wa 22 anayeishi naye hivi sasa ambaye miezi miwili iliyopita alikamatwa akitumia madawa ya kulevya.Amemzidi umri mume wake takriban kwa miaka 70.

Bibi Wook alisema kuwa angependa kusherehekea sikukuu ya Eid el-Fitr wiki hii akiwa pamoja na mumewe na kama ikibidi basi aolewe na mume mwingine ili amliwaze wakati wa sikukuu.Muhhamad alifunga ndoa na bibi Wook miaka mitatu iliyopita akisema kuwa urafiki wa karibu na heshima uligeuka kuwa mapenzi ya kweli. Eeh...Afadhali!

0 comments: