Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, March 21, 2010

Nazungumza na waajiri wangu (Wasikilizaji).
Ni wakati wa taarifa ya habari leo saa 6 na nusu mchana hapa Tokyo ambapo Afrika Mashariki ni saa 12 na nusu na Kule A. Kati saa 11 na nusu.

7 comments:

Anonymous said...

Huu ni wakati muafaka kwa redio Japani kuwa redio washirika nchini Tanzania ili wadau waendelee kufaidi matangazo yenu kwa raha zaidi.

Anonymous said...

Japani ni wadau wazuri sana wa maendeleo hapa Tanzania.Kwa hakika ni marafiki zetu wema sana.Mimi binafsi nawapenda sana katika utendaji wao wa kazi na misaada yao ya kijamii na utendaji wao wa kujitolea ndani ya jamii ya watanzania.Kwa uwezo wa mkubwa wa teknolojia wanaweza kufungua studio kwa ajili ya matangazo hapa Jijini Dar es salaam.Tafadhali sana tunaihitaji redio Japani nchini Tanzania ili tufaidike na redio iliyowekeza zaidi kwenye taaluma kuliko burudani.
"HII NI IDHAA YA KISWAHILI YA REDIO JAPANI IKIWATANGAZIA KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM NCHINI TANZANIA"Msomaji wenu ni Bakari Msulwa.
----------------------------------
Ray Ephraim Njau
Mdau wa redio Japani
Dar es salaam,Tanzania.
----------------------------------

Anonymous said...

Asante sana mdau wa redio Japani.
Hiyo siku itakuwa ya shangwe nderemo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kuanzia Kigamboni hadi Kitunda na Bunju hadi Mbagala.

Anonymous said...

Acha mchezo mtu wangu Wajapani wameng'arisha Tanzania kama mangi anavyong'arisha viatu.Majengo ya shule na mahospitali usiseme na juzi kati hapa balozi wao kasini mikataba ya misaada kwa wilaya kibao.Wajapani;we acha tu.

Anonymous said...

Naona Mr.Njau unaifagilia sana redio Japani ili iweke makazi nchini Tanzania.Au mzee unataka kuwa mtangazaji kama Bakari Msulwa?Acha utani naungana na mdau Njau katika mawazo yake.

Anonymous said...

Ipo Siku hilo litawezekana tu, tuvute subra.

Anonymous said...

IT TRUE,ONE DAY YES!!!!
RADIO JAPAN LIVE FROM DAR ES SALAAM TZ.WELCOME ALL!!!