Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, March 22, 2010

Eneo la Shibuya , katikati ya Tokyo hapa Japani.
Kuna aina hii ya uvukaji wa barabara baada ya kuwaka taa za kijani ambapo pande zote huwaka taa za kijani kwa pamoja na magari husimama hivyo watu huvuka . Inasaidia kuepusha ajali kama zinazotokea nyumbani ambapo mtu anavuka huku kule nyekundu mara puuuu...hivi hii haiwezi kutekelezeka kule kwetu..?

6 comments:

Anonymous said...

Asante sana kwa taswira kutoka Japani.Wahandisi kadhaa wa barabara zetu wanatoka Japani.Hapa suala la kuthubutu hasa wakati ambapo foleni zimeendelea kuwa kero kuu ndani ya Dar siti senta.

Anonymous said...

Nina hakika wajapani wakiambiwa kinachohitajika wanaweza kukifanya..Sioni ubaya wakachukua mbinu za wajapani za kupunguza ajali zikatafsiriwa kwa mazingira ya kwetu inaweza kusaidia. Jiji la Tokyo Watu Millioni 13 ajali za kizembezembe hakuna why us..ni mjadala unaohitaji kuzungumzwa.

Anonymous said...

Kupanga ni kuchagua kuendelea kujenga maghorofa bila miundo mbinu sahihi ya barabara na baadae kilio cha mtu mzima.Hakuna kisichowezekana ila ni nini vipaumbele vyetu.Wajapani wao wamedhamiria toka awali kuwekeza kwenye huduma za jamii na ndiyo maana kila kukicha kwao ni paradiso.

Anonymous said...

Na kweli lakini hatujachelewa, kama si sisi vizazi vyetu nadhani. Inabidi tuanzie mahali.

Anonymous said...

Wahandisi wa kitanzania kutwa nzima wako kwenye suti na tai.Je wanaweza kutuletea mabadiliko gani kwenye miundo mbinu?Wenzao wapo kazini saa 24 wakilinda taaluma zao kwa vitendo bila usanii.Huku bongo ajira za kurithishana kuanzia babu na sasa mjukuu kwenye ofisi ile ile kwa kuangalia vyetu vya kununua bila darasa kamili.Kwa mtazamo huo hakuna muujiza wa ubunifu na siku zote acha tubakie watu wa kushangaa.Kila mtu akifika ofisini anatunga sababu ya kuondoka ofisini akawakague mafundi wake kwenye maghorofa yake Kariakoo na mabanda ya kuku kule Kitunda.Maendeleo hayanyeshi kama mvua wadau!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

Hongereni sana wapajapani kwa kujali maisha ya watu wenu.