Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, March 20, 2010


Barabara inayopita katikati ya majengo ya Chuo Kikuu cha kilimo Tokyo...sehemu ninayokwenda.
Leo hapa kulikuwa na mahafali nami nilipita hapo na kufyatua chache kwa ajili ya mirindimo...


Chuo Kikuu cha Kilimo cha Tokyo hapa Japani



Kwa ndani..muonekano wake..

Wasomi hawa wametoka kuchukua Shahada zao mbalimbali za Kilimo , nikajipenyeza kupata picha ya Ukumbusho...ilikuwa safi ..tulifurahi na mabwana shamba wa Kijapani.


Shamba la mfano katika maandalizi ya mwisho mwisho , hapo utaalamu unazingatiwa kwa kiwango kikubwa...


Eneo la utafiti na Kilimo "shambani" hapa Tokyo ambapo uzalishaji unazingatia kanuni ya "mazao Mengi katika eneo dogo"

"Hodi zumbe!" Tafsiri yake ...Karibu katika makumbusho hayaya Chakula na Kilimo ya Kilimo. Maswaliiii..hamna!

Unapofika katika kituo cha Makumbusho ya kilimo "SUA" Tokyo utakutana na kitoweo hiki cha Picha.


Pembezpni wa "Jongwe" alama ya Makumbusho ya kilimo ya Chuo kikuu cha Tokyo.

2 comments:

Anonymous said...

Umakini wa wajapani katika shughuli zao ni somo zuri sana kwa wanazuoni kutoka nchi zinazoendelea.Ukitaka kufaidi zaidi shuguli za kilimo cha wajapani tembelea kule Yoyogi Park kwenye maonyesho ya kilimo.

---------------------------
R.Njau
Dar TZ.

BM. said...

Nashukuru Mr. Njau kwa comment yako kwahakika maonyesho nimeyaona ya Yoyogi Park , nawaza Tanzania yetu na Kilimo kwanza..tuna mengi ya kujifunza hapa kwa kweli.