Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, March 24, 2010

Mkutano wa kimataifa ulio chini ya Umoja wa Mataifa unaozungumzia spishi zilizo katika hatari ya kutoweka umekataa maombi kutoka Tanzania na Zambia kufanya mauzo ya mkupuo mmoja ya pembe za ndovu.Hebu bofya hapo uangalie ujangili huu unavyofanyika , halafu rejea kwenye mada . Jee wewe ungekuwa na kura ya turufu ungeamuaje kuhusu suala la kuruhusu au kutoziruhusu Tanzania na Zambia kuuza shehena zake za pembe za ndovu? Kwanza fuatilia suala hili lilivyochukuliwa nchini Kenya , nchi iliyoishikia bango Tanzania na kuwezesha ruhsa hiyo kukosekana bofya hapo.



Uamuzi huo umetolewa Jumatatu kwenye mkutano wa mataifa 175 huko Doha, Qatar. Biashara hiyo ingelikiuka marufuku ya kitaifa iliyowekwa mwaka 1989 juu ya uuzaji wa pembe za ndovu ili kuwalinda tembo kutokana na uwindaji haramu. Jason Bell-Leask, afisa wa mfuko wa kimataifa wa wanyama pori alisema tamko hilo ni ushindi nadra kwa tembo.
Tanzania na Zambia walisema idadi ya tembo wao imeongezeka kufikia kiwango ambacho wanaharibu mazao na kuuwa watu. Wapinzani walisema nchi hizi mbili zimeshindwa kuzuia uwindaji haramu wa tembo na uuzaji haramu wa pembe za ndovu. Tanzania iliomba kibali cha kuuza hifadhi iliyopo ya pembe za ndovu zenye thamani ya dola milioni 20. Zambia pia iliomba ombi kama hilo kisha ilijitoa na kupendekeza uuzaji wa sehemu zingine za tembo. Lakini meno hayo yanapatikanaje/ Bofya hiyo video hapo chini'

0 comments: