Mzee Nelson Mandela hakuonekana jana kwenye sherehe za ufunguzi w michuano ya Kombe la dunia ambapo Bafana Bafana ilitoka sare ya moja kwa moja na Mexico kufuatia kufiwa na Kitukuu chake kipenzi Zenani.Kitukuu cha Mzee Nelson Mandela , zenani (Pichani) amefariki dunia katika ajali ya barabarani akitokea katika moja ya shamrashamra za ufunguzi wa kombe la dunia.
Kufuatia tukio hilo Mzee Mandela ameshindwa kwenda mpirani na badala yake amejumuika na familia yake katika msiba wa kitukuu chake Zenani mwenye umri wa miaka 13 , na kuyafanya mashindano hayo kuwa na kihoro kiasi Fulani.
Msemaji wa Polisi katika jiji la Johannesburg Bi. Edna Mamonyane amesema kuwa dereva la gari lililomuua Zenani amekamatwa na atashitakiwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na kusababisha kifo.
Akiongea jana Jioni kwa saa za Afrika Kusini wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo Raisi wa Afrika Kusini Jacob Zuma alisema kuwa Mzee Madiba Mandela ameshindwa kufika uwanjani kutokana na msiba mkubwa ulioikumba familia yake.
Mtoto Zenani alikuwa kipenzi kikubwa cha Mzee Nelson Mandela miongoni mwa vitukuu tisa vya mzee huyo.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, June 12, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment