Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, July 04, 2010

Baadhi ya miili ya watu waliokufa kufuatia kulipuka kwa lori la mafuta huko DRC ikiwa imefunikwa , tayari kutambuliwa na hatimaye kuzikwa...

Zaidi ya watu 230 wanahofiwa kufa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo –DRC baada ya lori moja lilobeba mafuta lililokuwa likitokea Tanzania kuanguka na kuwaka moto katika kijiji cha Sange, mashariki mwa nchi hiyo.Inaarifiwa kuwa watu hao walikuwa wakijaribu kuchota mafuta kutoka lori hilo, lilokuwa limepinduka, baada ya dereva wake kushindwa kulidhibiti.Baadhi ya waliokufa walikuwa wakichota mafuta yaliyokuwa yakivuja, lakini walinaswa ndani ya majengo, ikiwa ni pamoja na ukumbi wa sinema.Walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliungana katika jitihada za kuokoa waliojeruhiwa.Walioshuhudia wanasema moto uliangamiza idadi kubwa ya nyumba.
Kijiji cha Sange kipo km 70 kusini mwa mji wa Bukavu, Kivu Kusini.Gari hilo lililokuwa likisafiri kutoka Tanzania, lilipinduka na mafuta kuanza kuvuja.
Madnodje Mounoubai, msemaji wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa, alisema idadi ya vifo huenda ikaongezeka.
Bila shaka tabia ya kukimbilia magari ya mafuta yaliyoanguka kwa lengo la kuteka mafuta inaangamiza roho za watu wengi barani afrika. Bado tunakumbuka ya Kenya, Tanzania , Uganda na Nigeria, Kulikoni wejemeni?

0 comments: