Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani Anna Kwambaza leo amefanya vyema wakati akiuimba wimbo wa Kijapani Tashika na koto , wakati akishiriki katika kipindi cha tuimbe kijapani , kipindi kinachotoa nafasi kwa watangazaji wa hapa RJ kuimba nyimbo za Kijapani kwa msaada na waalimu wa muziki.
Anna kwambaza ...
Anna alikuwa akiimba kana kwamba ni mwanamuziki wa muda mrefu na alimudu vipande vyote vilivyo na miteremko na milima na kujipatia sifa ya kuwa mmoja wa watangazaji wa kigeni kutoka Afrika aliyefanya vyema katika kipindi hiki.Unaweza kukisikiliza kipindi hiki kesho Jumamosi asubuhi kwa wale watazamaji wa MIRINDIMO wa Afrika Mashariki na wale wa Japani na barani Asia itabidi wasubiri hadi saa 7 kasorobo mchana hiyo kesho.Marekani kwa Da Subi na kule Ufini ...mtapima nyakati Mhhh .
Wimbo huo Tashika na Koto uliimbwa awali na mwanamuziki anayeitwa AZU lakini wanamuziki wengi waliuimba tena na tena...na hapa nimekuwekea wimbo huo huo lakini uliimbwa kwa mara nyingine na mwanamuziki wa kiume Oda Kazumasa.
Unaweza kusikiliza kipindi hicho kwa kubofya hapo kulia kwenye kifungu cha MARAFIKI , angalia hapo kulia chini utakutana na neno NHK WORLD SWAHILI -bofya hapo halafu endelea.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, October 01, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Asante kaka Bakari. Nitafuatilia.
Msulwa: Pongezi kwa dada yetu:
Post a Comment