Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, May 23, 2011

Mdada huyu nchini Marekani amefanya ukatili zaidi kwa kumuua kwa kumbanika kwenye Microwave mtoto wake mchanga wa mwezi mmoja eti kwakuwa mpenzi wake alikuwa haamini mtoto huyo ni wake.

China Arnold mwenye umri wa miaka 31 wa Ohio nchini Marekani amenusurika kuadhibiwa kunyongwa lakini amehukumiwa kutumikia maisha yake yote yaliyobakia jela bila ya kupewa nafasi yoyote ya kupata msamaha wa rais. China alikuwa na mzozo na mpenzi wake ambaye alikuwa akihoji mtoto mchanga aliyezaliwa na China kama ni wa kwake kweli au mwanaume mwingine.

Mzozo huo ulipopamba moto China alimchukua mtoto huyo aliyekuwa na umri karibia mwezi mmoja na kumweka kwenye Microwave na kuiwasha kwa dakika zaidi ya mbili.Waendesha mashtaka walisema kuwa kwa kukusudia kumuua mtoto huyo, China alimweka kwenye Microwave mtoto huyo mchanga wa siku 28 na alipoiwasha Microwave hiyo mtoto huyo alifariki kwa kuungua vibaya sana.

Ripoti ya madaktari ilisema kuwa mtoto huyo wa kike aliyepewa jina la Paris Talley alifariki ghafla baada ya joto la mwili wake lilipofikia kati ya nyuzi joto 43 Celcius. "Alifariki kwasababu aliwekwa kwenye joto kubwa sana, alikuwa kama amebanikwa", alisema daktari mstaafu Dr. Marcella Fierro.

Akitoa hukumua ya kesi hiyo jaji wa kesi hiyo alimhukumu China kwenda jela maisha akisema kuwa ukatili alioufanya ni zaidi ya ukatili wa mtu aliyeua kwa risasi au kwa kutumia kisu.
Chanzo; mtandao wa Nifahamishe

0 comments: