Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, April 03, 2009

Redi kapet inasuguliwa ...wakubwa karibu watapita hapo kwenda kula. Ukubwa una raha zake...

Posted by BM. on Friday, April 03, 2009

Mlo wa usiku baada ya kukamilisha mkutano wao wa siku Moja. Mataifa ishirini yaliyoendelea kiviwanda na yale yanayoibukia kiuchumi duniani .Afrika Kusini ndiyo taifa pekee barani Afrika lenye uanachama katika G20. Mada ya mkutano wa G20 ilikuwa kuutafutia ufumbuzi msukosuko wa uchumi unaoikumba dunia kwa wakati huu. Pia viongozi hao walijadili mbinu za kuzuia mdororo kama huu usitokee tena kwa siku zijazo.

Tunasubiri matokeo...

Posted by BM. on Friday, April 03, 2009


Malkia Elizabeth II akisalimiana na Bi Michelle Obama wanaoangalia ni Obama na Prince Philip. Uingereza Malkia ndiye mwenye nchi...alama ya taifa hilo..upooo!

Posted by BM. on Friday, April 03, 2009

Raisi wa Urusi Dmitry Medvedev na Raisi Barack Obama wakichati kabla ya Mkutano wa G-20.

Posted by BM. on Friday, April 03, 2009

Usiku wa wake wa wakubwa; Kutoka kushoto Ban Soon Taek, Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Chikako Aso Mke wa Waziri Mkuu wa Japani , Laureen Harper, Mke wa Waziri Mkuu wa Kanada , Gursharan Kaur, Mke wa Waziri Mkuu wa India ,Bi. Michelle Obama Mke wa Raisi wa Marekani, Kim Yoon-ok, Mke wa Raisi wa Korea Kusini, Sarah Brown,Mke wa waziri Mkuu wa Uingereza , Bi.Margarita Zavala Mke wa Waziri Mkuu wa Mexico na Bi. Svetlana Medvedeva mke wa Raisi wa Urusi, Emine Erdogan, Mke wa waziri Mkuu wa Uturuki ,Margarida Barroso,Mke wa Raisi wa Umoja wa nchi za Ulaya ,Therese Rein, Mke wa Waziri Mkuu wa Australia na Dr Pimpen Vejjajiva, Mke wa Waziri Mkuu wa Thailanda.

Posted by BM. on Friday, April 03, 2009

Stress ,kisayansi ninini!.....Sasa pata undani wa stress kwa kutumia uchambuzi huu wa kisayansi. Kwa hakika stress ni mkandamizo wa mawazo unaotokana na sababu mbalimbali.Pale unapopata tishio lolote lile mivumo yako ya ufahamu ya neva hujibu haraka kwa kutoa kitu kinachoitwa homoni za stress- stress hormones ambazo zina mchanganyiko wa adrenaline and cortisol. Homoni hizi zinauamsha mwili kwa hatua za hatari . Kuanzia hapo moyo wako utadunda sana, misuli itabana na kunakuwa na msisimko wa kutosha wa mwili. Mabadiliko haya yanakuongezea nguvu fulani na kukupa ujasiri wa kufanya maamuzi ya kujihami kwa haraka sana. Na ndipo hapo unajikuta ukikuta kitu cha kutisha unasimama ghafla na nywele zinakusimama. Kwa lugha nyepesi aina hii ya stress inajenga mazingira ya kukusaidia . Msaada huu una kikomo chake . Stress ikipita mstari Fulani inaanza kuleta madhara makubwa ya kiafya . Inavuruga furaha yako , mahusiano na hata kukusababishia magonjwa makubwa. Hivi unajua unaweza kupata kisukari , na hata kupunguza kinga ya mwili kwa kuwa na stress? Kwani unaweza kuidhiti vipi! Sasa soma Mirindimo ya Jumamosi kesho katika blog hii ujiepusha na balaa la stress sugu inayoweza kubadili rangi ya maisha yako!..

Posted by BM. on Thursday, April 02, 2009

Akina dada hawa wanaojiita wanaharakati wakiwa wanaandamana mitaani kama unavyowaona huko Uhispania kupinga mchezo wa kupambanisha madume ya Ng-ombe.Wanasema watu wanapowashangaa ujumbe unafika...haya ingekuwaje ingekuwa kwetu Manzese uwanja wa fisi ...sijui !


Posted by BM. on Thursday, April 02, 2009

Unapoingia unakula na kunywa na baadaye unaletewa bili unaambia chakula ulichokula , kinywaji na huduma ulizopata ni Dola Trilioni moja, millioni 243 laki 2 na 55 ,Upo!

Posted by BM. on Thursday, April 02, 2009

Zimbabwe hiyo ya Mugabe.....jamaa analipa bili. hiyo ni ya vinywaji kwanza ...bado ya vyakula na kazalika....Ni dola ya Zimbabwe kumbe...!

Posted by BM. on Thursday, April 02, 2009

Mtangazaji wa vipindi vya michezo wa Star Tv Hillary Riyami aliyekaa akitoa maelezo kwa mama mzazi wa Int.p.Peter Omar wa Kiss FM alipotembelea studio hizo hivi karibuni. ..................Inapendeza sana. ..........

Posted by BM. on Thursday, April 02, 2009

Mama wa IntP .Peter Omari Bi. Agnes Omari (katikati mwenye vitenge) baada ya kutembelea studio za Kiss Fm, RFA na Star Tv alikutana na kikundi cha comedy cha Star Tv kinachojulikana kama Futuhi .Safii.

.

Posted by BM. on Wednesday, April 01, 2009

Sherehe ya miaka20 ndani ya Ndoa ...Raisi Jakaya Kikwete na Bi Salma Kikwete. Hongereni....

Posted by BM. on Wednesday, April 01, 2009

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za dini nchini Tanzania Rose Muhando akiongea katika stesheni ya Kiss FM-Mwanza Tanzania . Kulia kwake ni Mwimbaji mwingine Bahati Bukuku..

Posted by BM. on Wednesday, April 01, 2009

Mtumishi wa Mungu Bahati Bukuku akiongea Kiss FM...

Posted by BM. on Wednesday, April 01, 2009

Waimbaji wa Nyimbo za dini..Rose Mhando (Kushoto) na Bahati Bukuku (Kulia) wakiwa na Mtangazaji na Meneja wa Kiss FM -Sahara Communication baada ya kurekodi kipindi kiitwacho Revival times kinachorushwa na kituo hicho kila J2.