Jioni ya leo Mie na mbongo mwenzangu Mr. Eustadius Francis (Anasoma Chuo Kikuu cha kilimo cha Tokyo)tulikwenda katika mgahawa wa Tsuraya eneo la Setagaya, mkabala na Chuo kikuu hicho kupata kikombe cha kahawa. Jambo lililotufurahisha sana ni kukutana na bidhaa ya tanzania ikinadiwa!
Kahawa ya Tanzania...pamoja na tangazo maalum kuelezea ubora wa bidhaa hiyo. Kwahakika ilibidi tuinunue na kula kile cha nyumbani...tulifarijika sana. Tulitamani kusema kwa sauti kuwa 'hii kahawa inatoka kwetu! '..pengine siku nyingine!
Hongereni wote waliofanikisha jambo hili...
Ni hapa...
Mwalimu wa Chuo cha Kilimo cha Mtwara Bw. Muhaji Abdallah Lenga (Pichani)yupo nchini Japani kuongeza ujuzi wa kilimo cha mpunga, kwasasa yupo eneo la Chiba. Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani ilibahatika kuongea naye. katika kipindi chote cha kuwa hapa Japani amekuwa akijibiidisha kwa nadharia na vitendo katika kujielimisha juu ya kilimo cha zao hilo.
Moja ya mambo yaliyonifurahisha sana katika mazungumzo yetu ni matumizi ya bata wakula magugu katika mashamba ya mpunga hapa Japani. angalia Picha za mabata hao wakiwa kazini.
Mwl . Lenga amesema kuwa Bata hawa ni chotara , mchanganyiko wa bata maji na bata kama wale wa nyumbani kwahiyo wanauwezo wa kuishi majini wakiwekwa huumo tangu upandaji wa mpunga hadi kuvunwa na baadaye hutumika kama kitoweo. Bata hawa wanafundishika na hawawaogopi binaadamu. Lengo la kuwatumia mabata hawa ni kupalilia mashamba kwa kula magugu na kuongeza mbolea kwa kinyesi chao. Hii ni mbinu ya kitaaluma ya kukwepa kutumia madawa ya kuuwa wadudu au kemikali.
Kemikali zina athari kubwa mashambani na kwa walaji. Kwa mujibu wa Mwl Muhaji, uzalishaji wa mpunga kwa kuwatumia mabata hawa ni wa gharama ya juu ,ikilinganishwa na ule wa matumizi ya madawa ya kuuwa wadudu ya viwandani.
Wajapani wanazingatia sana kanuni za kilimo na ndi maana wanapata mavuno mengi katika ekari moja..
Mdada wa Kiganda , Amani Wairimu na singo yake mpya ..Without you!
The washing machine cycle takes about 45 minutes – and George Washington comes out much cleaner in the Zimbabwe-style laundering of dirty money.Low-denomination U.S bank notes change hands until they fall apart here in Africa, and the bills are routinely carried in underwear and shoes through crime-ridden slums.
Some have become almost too smelly to handle, so Zimbabweans have taken to putting their $1 bills through the spin cycle and hanging them up to dry with clothes pins alongside sheets and items of clothing.It's the best solution – apart from rubber gloves or disinfectant wipes – in a continent where the U.S. dollar has long been the currency of choice and where the lifespan of a dollar far exceeds what the U.S. Federal Reserve intends.Zimbabwe's coalition government officially declared the U.S. dollar legal tender last year to eradicate world record inflation of billions of percent in the local Zimbabwe dollar as the economy collapsed.The U.S. Federal Reserve destroys about 7,000 tons of worn-out money every year. It says the average $1 bill circulates in the United States for about 20 months – nowhere near its African life span of many years.Larger denominations coming in through banks and formal import and export trade are less soiled.But among Africa's poor, the $1, $2, $5 and $10 bills are the most sought after. Dirty $1 bills can remain in circulation at rural markets, bus parks and beer halls almost indefinitely, or at least until they finally disintegrate.Still, banks and most businesses in Zimbabwe do not accept torn, Scotch-taped, scorched, defaced, exceptionally dirty or otherwise damaged U.S. notes.
-Huffpost World
Hatua moja huanzisha safari...
WATU wasiofahamika wamevamia shule ya kimataifa ya Livingstone ya wilayani Njombe mkoani Iringa na kumteka mwanafunzi mmoja wa kike katika shue hiyo na kumchinja kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.Imedaiwa kuwa watu hao ambao idadi yao haijafahamika walivamia shule hiyo majira ya saa 10 alfajiri ya kuamkia juzi na kuingia katika bweni la wasichana na kufanikiwa kumteka mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Doris Lutego (12) ambaye ni mkazi wa mtaa wa shule ya Uhuru mjini Makambako wilaya ya Njombe.
Wakizungumza kwa njia ya simu mtandao wa; www.francisgodwin.blogspot.com (Chanzo cha habari hii) na mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa kwa kuwa si msemaji wa juu wa tukio hilo alisema kuwa mwanafunzi huyo alitekwa usiku wa kuamkia jumapili na kuwa pamoja na jitihada za kumtafuta zilizofanywa na wananchi na viongozi wa shule hiyo jitihada zilishindikana .“Baada ya taarifa ya kuvamiwa kwa shule hiyo na kutekwa mwanafunzi huyo wananchi tuliendesha msako mkali wa kuwasaka wavamizi hao ila hatukufanikiwa hadi leo asubuhi baada ya wakazi wa eneo la kitongoji cha Kambarage Njombe kufanikiwa kukuta mfuko wa Salfeti ambao ulikuwa na mwili wa mtoto huyo ….mfuko huo ulikutwa nyuma ya nyumba ya balozi wa kitongoji hicho na baada ya kutafuta zaidi ndipo kichwa chake kilikutwa karibu na nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho huku kikiwa kimehifadhiwa katika mfuko wa madaftari ya mwanafunzi huyo”.
Hata hivyo alisema kuwa mbali ya kufanikiwa kukuta mwili wa mwanafunzi huyo ila bado hawajafanikiwa kuwakamata wahusika wa mauwaji hayo ya kinyama .Alisema kuwa mauwaji hayo yamewaweka katika maswali zaidi wakazi wa mji wa Njombe na wilaya nzima kwani inaonyesha wazi wauwaji hao wamefanya hivyo kama sehemu ya kulipiza kisasi katika familia ya mtoto huyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarit Mangalla (pichani) amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai kuwa mtoto huyo alikuwa akisoma darasa la tano katika shule hiyo .
Kamanda Mangalla alisema kuwa taarifa zilizofika polisi mapema jana zillikuwa ni za kutekwa kwa mtoto huyo na kukutwa kwa baadhi ya meno yake na damu katika kitanda chake na kuwa bado jeshi la polisi linafanya uchunguzi zaidi na kuwasaka wahusika wa tukio hilo.Nimeshikwa na uchungu...nimehuzunika sana.
Maelfu ya watu wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa bingwa wa michezo ya Olimpiki mbio za marathon raia wa Kenya Sammy Wanjiru jana Jumamosi aliyefariki mwezi uliopita baada ya kuanguka kutoka kwenye ushoroba wa nyumba yake. Mazishi yalifanyika katika kijiji cha Heshima, eneo la Ol joroonok na kuongozwa na mjane wa Marehemu Trizah Njeri-pichani akiweka shada la maua.

Hata hivyo mama mzazi wa wanjiru alitinga nyumbani kwa Marehemu akiwa na panga alilolificha kwenye mfuko akidai kuwa atamkata nalo mtu yoyote anayeunga mkono mazishi hayo.
Hata hivyo mazishi yalifanyika katika uwanja wa michezo katika wilaya alikozaliwa, Nyahururu, katika jimbo la Rift Valley, huko Kenya chini ya ulinzi mkali wa polisi. Mahakama iliamuru wiki hii kuwa Wanjiru, aliyekuwa na umri wa miaka 24, anaweza kuzikwa licha ya kuwa uchunguzi unaendelea kuhusu mazingira yaliyosababisha kifo chake na kusema kuwa Wanjiru alikufa ama katika ajali, au alijiua baada ya mkewe kumfumania na mwanamke nwengine. 
Mama yake Wanjiru, Hannah, alisusia mazishi hayo. Katika kile kinachoonyesha kupata heshima ya kitaifa alipigiwa saluti ya mizinga 21 wakati jeneza lake lilipoteremshwa kaburini katika shamba lake. Wanjiru alikuwa Mkenya wa kwanza kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki katika mbio za marathon za michezo ya Beijing mnamo mwaka 2008 na akihesabiwa kuwa mojawapo wa vijana chipukizi hodari.Mazishi yake yalihudhuriwa na wanariadha mashuhuri wa Kenya na watu mashuhuri. 





