Ni hapa...
Captain Dadis Mussa Kamara...
Muungano wa Umoja wa Ulaya, umetoa wito kuwa kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Kaptain Mussa Kamara afikishwe mbele ya Mahakama kukabili mashitaka ya ukiukaji wa haki za kibinadamu, wakati wa kuzuia maandamanoambayo yaliandaliwa vyama vya upinzani.Kwa mujibu wa mjumbe wa maendeleo ya umoja wa ulaya,Karel de Gucht, alisema yakuwa mkuu huyo wa jeshi,Kaptain, Mussa Kamara,anahusika na mauaji ya watu wasipungua 150, wakati walipouwawa, tarehe 28, Septemba,mwaka huu.Hata hivyo , kiongozi huyo anasema kuwa hahusiki na mauaji ya watu hao.
Vurugu za Konakri, Guinea na mabavu ya Dola!

Shirika Moja linalohusika na masuala ya Afya la Lung Foundation limesema kuwa watu millioni 6, watapoteza maisha kutokana magonjwa yanayosababishwa na uvutaji wa sigara, ifikapo mwisho wa mwaka ujao wa 2010.Limesema yakuwa watu wengi watakao athirika ni wale wanao toka kwenye dunia ya tatu au nchi masikini duniani kwakuwa uvutaji wa sigara katika bara la Amerika na za Ulaya na nchi nyingine zilizoendelea umepungua kwa kiasi, lakini uvutaji wa sigara umeongezeka katika nchi masikini. Eeeh Balaa!
Haya nakuunganisha na Dada Anyango , uone vipaji na jitihada za mdada huyu wa Kijapani . Nimekubali kuwa mambo mengi yanawezekana la msingi dhamira...
Ama kwa hakika , tumetoka mbali ..we acha tu.Leo nakuchukua hadi Rungwe Sekondari , shule iliyopo wilayani Rungwe , mkoani Mbeya kwa njia ya picha... nikuonyeshe shule niliyosoma, . picha kwa hisani kubwa ya Bro. Mwambegele.
Hapo Kiwira mwankenja ni kilometa 15 tu kutoka Tukuyu Mjini. Km kama mbili tu kutoka hapo utaona kibao kinachokuonyesha njia ya kwenda shuleni kwetu!
Ehee hapo chepuka kulia moja kwa moja hadi Rungwe Sekondari ,chini ya Mlima Rungwee!
Mbele ya jengo hilo ndio muonekano wa Mbele , ambako kila asubuhi tulikusanyika hapo kuelewa majukumu ya siku, kukaguliwa usafi. "Asembli". Na mwanzoni mwa mwaka kuna wengi walikuwa wakiadhibiwa hapo kwa kuwabughudhi "Mugya" , jina walilokuwa wakiitwa wanafunzi wa kidato cha kwanza. Sijui leo pakoje hapo!
Ofisi za waalimu ghorofani na madarasa hapo chini...inanikumbusha mbaali.
Wale wapenzi wa Rhumba la kutotoa jasho wanaweza kubofya hapo wakaburudika na tungo za Koffi Olomide.... Jamaa kajipanga au unasemaje!
Jana Jumapili kulikuwa na Maonyesho ya bidhaa za mashambani hapa Tokyo , Japani na katika pitapita yangu nikakutana na banda lina kanga , vitenge , kahawa na bidhaa nyingine kutoka Tanzania. Banda hili ni la Polepole, kamera yangu ikapata hii...
Hapo nimekutana na Mr. Tamura , Mkuu wa banda la Polepole linalouza bidhaa za Tanzania. Tumezungumza sana akinipa hadithi za Moshi na Arusha anasema "Kule safi saaana". Watu kama hawa wanaoitangaza nchi yetu wanastahili kutambuliwa na kuheshimika sana...wahusika mnasemaje!
Kahawa kutoka umatengoni...Mbingaa aisee!
Sabuni za mwarobaini zilikuwepo!
Wikiendi kulikuwa na zoezi la jinsi ya Kujiepusha na majanga kama vile matetemeko, moto na majanga mengine lililofanyika katika Uwanja wa Yoyoygi hapa Tokyo nami nilishiriki ...
8.8 nikiwango che ukubwa wa tetemeko ...mtikiso mkali mithili ye tetemeko kutoka kwenye gari maalum. Wataalamu wakitoa maelekezo jinsi ya kufanya...du!
Tetemeko linaposhika kasi unafanyaje? Sasa zoezi la moto...
Huu ni mfano wa nyumba...Moto umewaka na ndani kuna moshi mwingi unafanyaje...wataalamu wanasema kuwa monyi unatabia ya kushika sana juu kwanza hivyo chuchumaa na ikibidi tembelea kifua unaweza kusalimika. Wacha nijaribu...
Nimetembelea kifua ndani kwa ndani na kutoka!
Ilikuwa tarehe mosi may, 1961 Pale Nelson Mandela, alipoonyesha msimamo wa kupambana na ubaguzi wa rangi na ndipo mwandishi wa habari wa shirika moja la habari la ITN Brian Widlake alipomfuata kwa minajili ya kufanya naye mahojiano. Unaweza kuona Ushupavu wa uthabiti wa viongozi wa Nyakati zile na viongozi wa sasa na nini changamoto zetu...













