Kenneth Douglas, 55, alitumia mwanya wa zamu yake ya masaa 16 usiku kuMfanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika jimbo la Indiana nchini Marekani amehukumiwa kifungo baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na maiti zaidi ya 100 katika monchwari aliyokuwa akifanya kazifanya mapenzi na maiti za wanawake.Douglas alikuwa akilewa sana pombe au madawa ya kulevya wakati akifanya uchafu wake huo ambao uligundulika baada ya polisi kufanya uchunguzi wa DNA.Douglas tayari anatumikia kifungo jela baada ya kukiri kufanya mapenzi na maiti ya msichana aliyekuwa amechinjwa, Karen Range ambaye alikuwa na umri wa miaka 19 wakati alipouliwa mwaka 1982.Hivi sasa Douglas anakabiliwa na mashtaka mawili mengine kama la mwanzo baada ya wachunguzi kupata ushahidi wa Douglas kufanya mapenzi na maiti za wanawake wawili waliouliwa mwaka 1991.Polisi wanaamini kwamba idadi ya miili ya wanawake iliyochezewa na Douglas inazidi 100 huku yeye mwenyewe amedai hakumbuki idadi yake."Huyu si mtu ni nguruwe. Siwezi kuelezea kitendo kama hicho alichokifanya cha kufanya mapenzi na maiti" mwendesha mashtaka aliiambia mahakama."Hatutaweza kujua idadi kamili ya wanawake aliowafanyia mchezo wake mchafu kwakuwa hata yeye mwenyewe hajui idadi yake". alisema mwendesha mashtaka huyo.Polisi walianza kuchunguza shughuli za Douglas baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na maiti ya Range mwaka jana.Polisi waligundua miili mingine 15 baada ya hapo ikiwa imeishafanyiwa mchezo mchafu wa mfanyakazi huyo wa usiku wa monchwari na kufanikiwa kupata ushahidi wa DNA katika miili miwili.Mojawapo ya miili hiyo miwili iliyotoa ushahidi mzuri wa DNA ni mwili wa mwanamke aliyekuwa na mimba ya miezi sita Charlene Edwards, aliyeuliwa mwezi oktoba mwaka 1991.Douglas alihukumiwa kwa kosa la jinai kwa kutumia ushahidi wa DNA uliopatikana kutoka kwa mwanamke huyo aliyefariki miaka 18 iliyopita.
Ni hapa...
Madaktari wanapokata tamaa........
Nyota wa vipindi vya televisheni Uingereza, Jade Goody ambaye aliolewa mwishoni mwa wiki baada ya madaktari kumwambia kuwa ana siku chache za kuishi kutokana na saratani yake kufikia pabaya amesema kwamba sasa yuko tayari kuelekea peponi.
Jade alifunga ndoa na mpenzi wake Jack Tweed katika harusi iliyofana sana mwishoni mwa wiki ikiwa ni siku chache baada ya madaktari kumtaarifu Jade kwamba kansa yake imefikia hali mbaya na kwamba nyota huyo ana wiki chache tu za kuishi kabla hajafariki.
Jade alizikusanya nguvu zake zote na kufanikiwa kusimama na kudansi kwenye harusi yake pamoja na hali yake kuzidi kuwa mbaya.Mume wa Jade, Jack Tweed ambaye bado anatumikia kifungo cha nje akitakiwa kuwa nyumbani kwa familia yake kabla ya saa moja usiku kila siku, alipewa idhini maalumu na Jack Straw kutumia usiku mmoja wa harusi yake na mkewe.Jack Tweed alifungwa miezi 18 mwaka jana baada ya kumshambulia kijana mmoja wa miaka 16 na gongo la mpira wa gofu, lakini sasa ametolewa jela akiendelea kutumikia kifungo chake nje.Jade, mama wa watoto wawili alishindwa kabisa kuficha huzuni yake aliporudi nyumbani kwake akiwa anatokwa na machozi huku akisaidiwa kutembea na mumewe na msaidizi wake.
"Amechoka sana , harusi ilikuwa nzuri sana lakini imemfanya achoke zaidi" alisema mama yake Jackiey Budden."Nilifanikiwa kutumia siku yenye furaha zaidi kuliko zote katika maisha yangu" Jade aliliambia jarida la OK! na kuongeza kwa kusema kuwa "Sasa nipo tayari kuelekea peponi".Jade aliuza hati miliki za harusi yake kwa paundi milioni 3 ambazo alisema ataziweka katika mfuko wa kuwatunza wanae wawili Bobby,5, na Freddy, 4.Jade aligundulika ana saratani wakati alipokuwa akishiriki Big Brother ya India inayojulikana kama Big Boss mwaka 2008.Jade alirudi Uingereza na kuanza matibabu katika hospitali ya Royal Marsden Hospital iliyopo jijini London.
Jade aliamua kufunga ndoa na mpenzi wake Jack Tweed siku chache baada ya kuambiwa atafariki katika wiki chache zijazo kwakuwa ugonjwa wake umefikia hatua ambayo hauwezi kutibibika tena. Fuatilia picha hizi Jade akiwa katika hali ya kawaida mitaani…hadi sasa akisubiri siku ya kifo chake…ni ngumu ! unasemaje …Fuatilia picha zake
Rio Carnival imeanza rasmi jumatatu baada ya kufunguliwa rasmi na rais wa Brazili aliyeamua kugawa kondomu ili washiriki na wahudhuriaji wajilinde na ugonjwa wa ukimwi.Rais wa Brazili ameamua kuonyesha jinsi anavyounga kampeni za kupunguza ugonjwa wa ukimwi nchini Brazili kwa kuwagawia kondomu watu wanaoshiriki na wanaohudhuria Rio Carnival.Rais Luiz Inacio Lula da Silva aliwarushia kondomu watu waliohudhuria Rio Carnival wakati wa ufunguzi wa Carnival hilo maarufu na kubwa duniani.Msemaji wa rais huyo alisema kwamba Rais Silva alitaka kuonyesha umuhimu wa kampeni ya Brazili ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.Mwezi huu pekee Brazili itagawa jumla ya kondomu milioni 65 ikiwa ni zaidi ya kiwango cha kawaida cha kondomu milioni 45.Brazili mwaka huu in mpango wa kununua kondomu bilioni 1.2 na kuifanya iwe serikali inayoongoza kwa kununua kondomu nyingi duniani.Carnival la Rio linalofanyika kila mwaka kwa siku tano mfululizo limeanza rasmi jumatatu likishirikisha vikundi kadhaa vya ngoma na maonyesho na kuhudhuriwa na watazamaji zaidi ya 80,000 katika uwanja wa Sambadrome jijini Rio de Janeiro.
Waandishi wa habari waandamizi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari walikutana Morogoro Mwezi wa pili mwaka 2008 mjini Morogoro , kujadiliana Juu ya mwenendo wa mfuko wa BIma ya afya . Picha muhimu za kumbukumbu ya tukio hilo.
Pichani ...kufahamiana na Mhariri wa Kituo cha TV Channel 10 ni muhimu. Nyuma yetu ni paparazi Charles Hillila wa Channel 10 Kituo cha Shinyanga. Nami Nikiwakilisha TBC ....Mkoa wa Shinyanga. inapendeza.
Mwanaume mmoja mwenye wivu amemuua mkewe baada ya mkewe kutaja jina la mwanaume mwingine wakati wakifanya tendo la ndoa. Colin Scully,53 amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Leeds, Uingereza baada ya kumuua mkewe Tracey,39 kwa kumniga koo lake kutokana na wivu baada ya mkewe kutaja jina la mwanaume mwingine wakati wanafanya mapenzi.
Inasemekana kwamba Colin alikuwa akishuku mkewe anatoka nje ya ndoa baada ya kufanikiwa kusoma ujumbe wa simu katika simu ya mkewe lakini akaamua kufanya uchunguzi wake kimya kimya.Pamoja na jitihada zake Colin hakufanikiwa kupata ushahidi wa kuthibitisha kutoka nje kwa mkewe.Inasemekana usiku mmoja wakati wanafanya tendo la ndoa mkewe kwa bahati mbaya akamwita mumewe "Paul" jina la mwanaume mwingine.
Paul hakuwa mwingine bali ni Paul Daigton rafiki wa mkewe ambaye wako pamoja katika klabu yao ya scooter.Colin kwa hasira alimkamata mkewe shingoni na kumkandamiza kwa nguvu kwa muda mpaka alipoona mkewe hatingishiki na kumuacha na kwenda kulala chumba cha watoto wao.Inasemekana kwamba asubuhi wakati Colin akijiandaa kwenda kazini ndipo alipogundua kwamba alimuua mkewe na kuamua kupiga simu polisi "Nimemfanyia kitu mke wangu, sijui nimefanya nini".
Polisi walipofika eneo la tukio walimkamata Colin na baada ya maiti kufanyiwa uchunguzi iligundulika kwamba marehemu alifariki baada ya kukandamizwa shingoni kwa muda mrefu.Kesi yake itaendelea kusikilizwa kwenye mahakama hiyo. imekaaje hii..