Ni hapa...
Leo Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani -NHK World ilitembelewa na mdau muhimu, Dr.Kamugisha Kazaura, ambaye wakati fulani alikuwa nasi katika kusukuma jahazi hapa jengoni. Kwasasa ana majukumu muhimu ya kitaifa kule nyumbani Tanzania. Sote tulifurahi kuwa naye!.
Pamoja na mazungumzo marefu , alitukabidhi mzigo kutoka kwa 'Babu' , alituambia tunywe inafanana na 'ile'. na baadaye tulipiga picha ya ukumbusho wadau tuliokuwepo wa Swahili service!
Shukran Mkuu, kila la kheri...
Maafisa wa kijeshiwa Uingereza wakisema wamefanikiwa kuuvuruga kabisa mfumo wa jeshi la anga la Libya katika mapambano yao yanayowashirikisha mataifa kadhaa ya Magharibi ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Marekani, Uingereza na baadhi ya mataifa ya kiarabu.Mashambulizi ya hivi karibuni yaliendelea huku milio ya makombora ikifyatuliwa kwa mfululizo.
Operesheni hiyo inatekelezwa, wakati ambapo wajumbe kutoka nchi 28 za jumuiya ya Kujihami ya NATO, wakiendelea na mkutano wao nchini Ubelgiji, wenye lengo la kujadili namna jumuiya hiyo itakavyoshiriki katika operesheni hiyo. Hali bado ni tete libya. Unaweza kuona pilikapilika za waasi wa Serikali ya nchi hiyo wanaosaidiawa na Nchi za magharibi.
Unaweza kufikiria ukali wa mawimbi ya tsunami ulivyokuwa...meli imepandishwa juu ya ghorofa ya pili ya makazi ya mji huu ...inatisha.
Jitihada za kuwatafuta watu bado zinaendelea ...zaidi ya watu elfu 30 wanahofiwa kufa ingawa idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi. (Mpiga mbizi akijaribu kutafuta miili ya watu chini ya bahari katika fukwe za bandari ya Ayukama, Ishinomaki)
Mwanaume mmoja nchini Japani aliyekiri kuwaua watu saba jijini Tokyo, mwaka 2008 kwa kuendesha gari kwa kasi kwenye mtaa wa watu wengi na baadaye kutumia kisu kikali kuwamaliza wengine amehukumiwa adhabu ya kifo.
Tomohiro Kato aliendesha gari kwa kasi katika eneo la watembea kwa miguu katika mji wa kibiashara wa Akihabara uliopo katikati ya jiji la Tokyo na kupoteza maisha ya watu watatu pale pale. Kisha akatoka garini akiwa na kisu kikali na kuanza kuwachoma watu ovyo na kuwauwa watu wengine wanne .Wakati wa kesi yake, Kato mwenye miaka 28 alisema kuwa alichukizwa na unyanyasaji uliokuwa ukifanywa kwenye mtandao lakini kilichofanya Mahakama Kuu ya wilaya ya Tokyo imuhukumu kifo ni matamshi yake kuwa “Yeye anahusika na alifanya kwa makusudi shambulizi hilo lililouwa watu.
Jaji Hiroaki Murayama alisema kuwa mtu huyo aliwashambulia kwa kisu mtu yoyote aliyemsogelea baada ya kuzungukwa na hivyo kuleta mazingira yaliyohatarisha maisha ya watu ambao hawana hatia.Alisema kuwa ni tendo la jinai lililo na ukatili mkubwa .
“Sina kingine cha kuchagua zaidi ya kumuhumu adhabu ya kifo” , alisema Murayama.
Mwandishi wa habari Jonas Jackson Songora , majuzi alitunukiwa shahada yake ya Pili (Degree of master of Science in International Cooperation policy) katika Chuo Kikuu cha Ritsumeikan Asia Pacific-APC baada ya kutimiza vigezo vinavyohitajika. Sherehe ya kutunukiwa nondozz hizo ilifanyika Jumamosi ya tarehe 16 , March katika Chuo hicho kilichopo eneo la Kyushu Kusini mwa Japani. Kabla ya kuja hapa Japani Jonas aliwahi kufanya kazi nchini Tanzania katika vyombo mbalimbali vya habari (Redio na Magazeti) na kwasasa anawajibika katika Shirika la Utangazaji la Japani -NHK world) Idhaa ya Kiswahili, kama mtangazaji wa kutumainiwa.
Picha; ya kwanza ameshikilia cheti chake, inayofuata akiwa na wahitimu wenzake , chini yake na wanafunzi wa kiafrika wanaosoma hapo na mwisho mwanafunzi mwenzake wa kitanzania Moses Kwabhi..
Hongera sana bro!
Shirika la Utangazaji la Japani -NHK World kupitia kituo chake cha televisheni -Channel 1 kesho saa tatu usiku hadi saa nne usiku (Kwa saa za Japani) sawa na saa tisa hadi saa 10 jioni(Kwa saa za Afrika Mashariki ) Litatangaza kipindi maalum cha tetemeko kubwa la ardhi na baadaye mawimbi ya tsunami , maafa yaliyotokea Ijumaa iliyopita.
Kipindi hicho kitaonyesha hatua kwa hatua hali ilivyokuwa, hatua zilizochukuliwa na hapa tulipofika.Jipatie fursa ya kujionea kile kilichotokea. Si vibaya ukamweleza mwenzako juu ya taarifa hii...
US President Barack Obama has said Libyan government forces must end their offensive against rebel-held towns and pull back - or face military action.He said the terms of a UN Security Council resolution backing action to defend civilians were "not negotiable".
Col Muammar Gaddafi's government has declared a unilateral ceasefire, as attack plans are drawn up against him under the UN resolution.There are reports government offensives are continuing despite the ceasefire.Libyan officials have dismissed these as untrue and say international observers are being invited to Libya to verify the situation.In the rebel-held western city of Misrata, which is surrounded by government forces, residents there told Reuters news agency that there was no sign of a ceasefire and that the city continued to be pounded by bombs and artillery. And Arabic TV station al-Jazeera reported that pro-Gaddafi forces were advancing quickly towards the eastern rebel stronghold of Benghazi on Friday evening. Its correspondent reported that loyalist forces were clashing with rebels in the towns of al-Magroun and Slouq, about 50km (30 miles) from the city.
Mr Obama said: "All attacks against civilians must stop. Gaddafi must stop his troops from advancing on Benghazi, pull them back from Ajdabiya, Misrata and Zawiya, and establish water, electricity and gas supplies to all areas."Humanitarian assistance must be allowed to reach the people of Libya.
"Let me be clear, these terms are not negotiable. If Gaddafi does not comply, the international community will impose consequences, and the resolution will be enforced through military action."Our goal is focused, our cause is just and our coalition is strong."
The US ambassador to the UN, Susan Rice, told CNN that Col Gaddafi was in violation of the UN Security Council resolution, adopted on Thursday, which called for an immediate ceasefire and banned all flights over Libya.But Libya's Deputy Foreign Minister, Khaled Kaim, said on Friday evening that Libyan government forces had conducted no military operations since announcing the ceasefire earlier.
"We have had no bombardment of any kind since the ceasefire was declared," he told reporters when asked about reports of continued government operations in Misrata and other parts of the country.
'Actions not words';
US Secretary of State Hillary Clinton is travelling to Paris on Saturday to join allies in discussing the next steps in Libya. (Source BBC)
Ubalozi wa Tanzania Japani unapenda kuwajulisha kuwa umeendelea kupokea taarifa kutoka mamlaka za Serikali ya Japan kuhusu hali inavyoendela kufuatia hitilafu ya mitambo/vinu vya kufua nuklia iliyotokea na inayoendelea kutokea katika mkoa wa Fukushima, pamoja na matetemeko yanayoendelea. Ubalozi umehakikishiwa kwamba bado maeneo mengi ni salama, ukiacha maeneo ambayo yapo umbali wa km 20 kutoka katika mitambo hiyo (exclusive zone) na km 20 hadi 30 ambako watu wamepewa maelekezo ya kukaa ndani.
Aidha, Ubalozi umejulishwa kuwa, pamoja na kwamba mionzi ya nuklia kutoka kwenye vinu hivyo imeweza kusambaa hadi maeneo mengine kama Tokyo, Kanagawa, Kawasaki, Ibaraki n.k., kiwango kilichopo ni kidogo sana kuweza kuleta madhara kwa afya ya binadamu.
Pamoja na taarifa hizo zilizotolewa na Serikali ya Japan kuwa hali ni salama, Ubalozi unawaomba Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari zaidi. Hivyo, unatoa rai kwa Watanzania wote wanaoishi Japan kutoa ushirikiano ili Ubalozi uweze kuweka rekodi zao kwa usahihi (up-date information), ukizingatia kwamba baadhi walisharudi Tanzania, wengine wamehamia katika maeneo mengine na wapo pia waliobadilisha namba zao za simu. Taarifa hizo zitausaidia Ubalozi kufanya mawasiliano ya haraka na kila mtu endapo hali ya kiusalama itakuwa mbaya na kulazimu tahadhari za ziada kuchukuliwa
Hivyo tunaomba kila Mtanzania atume taarifa zifuatazo kwenye anwani za Ubalozi zitakazotajwa hapo chini.
Jina kamili, Orodha kamili ya familia yako (kama unaishi na familia), Anwani ya mahali unapoishi (mtaa/mji/eneo n.k.), Namba za simu unazotumia (mobile phone/residential)mawasiliano yake ikiwa ni pamoja na jina, simu/email, anuani yataa, n.k.
Ubalozi unaomba ushirikiano wenu, na kila upatapo ujumbe huu tafadhali mjulishe na mwenzako.
Tafadhali tunaomba taarifa hizo zitumwe kwenye anuani pepe zifuatazo
jmaleko@tanzaniaembassy.or.jp , fmossongo@tanzaniaembassy.or.jp , tzrepjp@tanzaniaembassy.or.jp , tzrepjp@gol.com
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania, Japan.
16/03/2011
Wasiwasi wa kutokea upungufu mkubwa wa chakula hasa kilichokwisha pikwa nchini Japani umewafanya watu kukimbilia madukani na kununua vyakula kwa wingi tangu Ijumaa iliyopita tetemeko lilipotokea. Leo maduka mengi ya vyakula yana vyakula vichache ,hakuna maji ya kutosha ya chupa na maziwa ya paketi yamekuwa adimu. Bidhaa zilizobakia kwa wingi ni biskuti na vikaukau.
Vijikabati vya maduka ya vyakula na bidhaa nyingine ya kujihudumia ( supermarkets ) na madogo maarufu katika jiji la Tokyo kama ‘convenience vilikuwa havina bidhaa za kutosha . Bila shka msongamano wa magari umeifanya kazi ya kusambaza bidhaa za vyakula katika maduka hayo kuwa ngumu na ya kukatisha tamaa.
Tetemeko la Ijumaa pia limesababisha hasara kubwa madukani kwa bidhaa nyingi kuanguka na kupondeka hususan zilizopangwa karibu na vimimika , vinywaji baridi na moto. Ukosefu wa umeme katika baadhi ya maeneo na pia mgao wa umeme ambao unashuhudiwa kwa mara ya kwanza katika miongo mingi bila shaka umeshusha uzalishaji wa vyakula vya kusindika vinavyotumiwa sana Japani na sekta ya usafirishaji kutoka kwa wakulima hadi kwa mlaji imevurugika kwa kiasi fulani. Maji ya kunywa ya chupa yameadimika madukani , wasiwasi ukisababishwa na taarifa za kukatika kwa maji katika baadhi ya maeneo kutokana na kuvurugika kwa miundomsingi.Hata hivyo mgao huu wa umeme unafanyika kisayansi sana na ni vigumu watu wanaoutumia umeme wa kawaida kuhisi athari zake kubwa. Inakuwa mchana kwa dakika kadhaa na bila shaka kutokana na baadhi ya viwanda kusitisha uzalishaji hiyo pia imesaidia.
Katika miji iliyopo katika viunga vya Tokyo, Kyodo na chitosefunabashi , maduka mengi yalifungwa jana (J4) lakini yamefunguliwa leo na jana watu walionekana kuwa katika kasi ya kurejea nyumbani. Pengine tatizo linalowakuta wageni ni kutoelewa matangazo yanayowkwa kwenye mbao za maduka kwa lugha ya kijapani...lakini bila shaka itakuwa ni mgao wa umeme au hadhari ya tetemeko.
Watu waliekea kwa wingi katika Jiji la Ginza kununua bidhaa za vyakula na katika kipindi kifupi maduka yalibaki tupu. ‘Vyakula sasa vinahamia majumbani badala ya kukaa madukani’, mtu mmoja raia wa Marekani aliyejitambulisha kwa jina la James alimfahamisha mwandishi wa habari hizi akiwa anafanya manunuzi katika eneo la Shibuya katikati ya Tokyo
Matetemeko yamekuwa yakiendelea hapa Japani kuanzia Ijumaa iliyopita na Shirika la utabiri wa hali ya hewa la Japani limeonya kuwa litatokea tetemeko jingine kubwa la mfuatizo wa tetemeko lililotokea ijumaa iliyopita na kusababisha mawimbi makubwa ya tsunami.
Mpaka sasa kwa ujumla wake shirika hilo limesema kuwa matetemeko madogo zaidi ya 50 yamekwishatokea Japani nzima yakiwa na ukubwa wa 3 hadi tano kwa kipimo cha richa . Wasiwasi uliopo ni kutokea kwa tetemeko lenye ukubwa wa 6 hadi 7 kwa kipimo cha richa kati ya leo jumanne na keshokutwa alhamisi.
Habari za hivi karibuni kutoka Shirika la Polisi la Japani zinasema kuwa watu Elfu 10 hawajulikani walipo , mawasiliano kati yao na ndugu zao hayapo, hawamo katika idadi ya miili iliyotambuliwa. Bado miili ya watu 200 na zaidi haijatambuliwa na hivyo idadi ya watu waliopotea huenda ikafikisha idadi kamili ya waliokufa kuzidi elfu 10.
Watu wengi waliokolewa wanahifadhiwa katika vituo maalum na kupatiwa maji na chakula na waokozi zaidi ya laki moja wengi wakiwa wanajeshi wa Japani wanashiriki katika zoezi hilo. Nchi 69 duniani zinashiriki katika zoezi hilo la Uokozi, ambapo Marekani inatumia ndege zake maalum za uokozi kujaribu kuwaokoa watu walionasa kwenye vifusi.
Taarifa za karibuni za mtandao wa NHK zinabainisha kuwa watu 19 wamebainika kupoteza maisha kutokana na mnunurisho wa nyuklia na jitihada zinafanywa kuzuia janga hilo lisisambae kwa watu wengi na idadi ya watu waliohamishwa mpaka sasa inatajwa kuwa ni 399.
Hata hivyo idadi kamili ya waliopoteza maisha yao, waliojeruhiwa na kupotea hadi sasa itatangazwa na vyombo vya habari vya hapa muda mfupi ujao. Polisi katika eneo la Iwagi wameonekana katika eneo lililo na kinu cha nyuklia wakiwa wamevaa barakoa(Masks).
Katika jiji la Iwaki watu anahama kwasababu kadhaa ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa vyakula madukani kulikosababishwa na maafa na Polisi wa eneo hilo wamekuwa wakiwagawia wakazi hao matonge ya wali 'maarufu hapa kama 'onigiri' na maji.
Wakati huo huo Shirika la Utabiri wa hali ya hewa la japani limesema kuwa tetemeko la Jana Ijumaa lilikuwa na ukubwa wa 9.0 na sio 8.9 kwa kipimo cha matetemeko cha richa.
Hakuna umeme wala maji. (Unaweza kuzipata habari zaidi kupitia Associated Press)
Many of us have, at one time or another, experienced a “late night eating” pattern. This is a very common behavior that is seen during periods of anxiety, depression or lowered self-esteem. A night eating syndrome is defined as when we consume at least 25- 50% of our daily calories after dinner time on a regular basis.
While the occasional late night eating or snacking is fine, provided you choose healthy foods and not heavy, greasy or highly sugared foods, persistent late night eating can cause problems for the digestive system and for your ability to sleep well. Studies at the Weill Cornell Medical Center show that people who eat late at night eat more calories than they would if they were eating during the daytime. This does not bode well for the work your digestive system has to do while you are sleeping or for calorie and weight management.
In addition, eating late into the evening can offset how well your body is able to rest, repair and recharge. When the body is busy digesting, absorbing and assimilating nutrients at night rather than taking the necessary rest and healing the body requires during sleep hours, you can wake up feeling fatigued and out of sorts.
Here are some ideas of how to avoid late night eating and create healthy habits:
• Eat a large dinner before 6:00 PM. This will give you a feeling of fullness, reduce late night hunger and prepare your body to slow down and get ready for a good nights sleep.
• When you feel the urge to eat late at night, eat or drink something low in calories that will provide both emotional and physical nourishment. A packet of hot, instant oatmeal is delicious, filling and only 150 calories.
• If you have allowed yourself to get into the habit of eating late, you can start slowly to change that by reducing the amount of food you eat each evening and then choosing more plant based and natural foods to consume which will healthier, more nutritious as well as lower in calorie intake.
• Do not eat processed foods, white flour or sugar or “treats” after 6:00 pm. These foods can cause spikes and drops in your sugar levels and lead to late night hunger.
• An interesting strategy is brushing your teeth earlier in the evening. Many people find that after they brush their teeth they are not as likely to consume more food because the do not want to have to repeat their dental hygiene routine over again.
• Exercise in the evening, in place of TV watching, is a wonderful blood sugar regulator that allows not only for better digestion, increased calorie burning, more toned muscles and a deeper sleep, but it also prevents getting triggered by TV commercials to want to eat more. Late night eating is something we should all avoid, apart from the occasional indulgence, to keep our bodies functioning and healing at its best during our sleeping hours.
Source: Dr. Georgianna Donadio, dailystrength.org, February 25, 2011
The work of Dr. Georgianna Donadio DC, MSc, PhD has touched the lives of millions of people worldwide. For more than 35 years, she has been educating the healthcare community, as well as her patients, students and the public
Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani , Bw. Francis Mussongo ametoa wito maalum kwa watanzania wanaoishi nchini Japani kuchukua hadhari kufuatia habari za kuvuja kwa mnunurisho wa nyuklia. Hii ni taarifa yake kamili;
Ndugu watanzania mliopo Japani,
Kwa Mujibu wa taarifa zinaendelea kutolewa na NHK Japan, mitambo ya Nuclear Fukushima Plant (1) kuanzia saa 10 jioni kwa muda wa Japan inatoa radiations na kuna dalili za mlipuko katika kituo hicho, Hali hii imepelekea kutangazwa kwa hali ya dharura na watu wote wa maeneo hayo wanatangaziwa kuondoka maeneo ya karibu na eneo hilo ili kuepusha madhara endapo hali hii itaendelea. Endapo mlipuko utatokea kuna uwezekano wa kuleta madhara kwa watu na mali hadi umbali wa kilomita 10 kutoka eneo la Kinu hicho cha Nyuklia. Kwa kutambua kuwa kuna watanzania wenzetu katika eneo la Fukushima kupitia mtandao huu tunaomba wenye mawasiliano na wenzetu waliko Fukushima kuwajulisha kuondoka katika maeneo hayo. Tahadhari pia inatolewa pia maeneo ya Fukushima kuna uwezekano wa kutokea Tsunami tunashauri wenzetu waliko huko wajulishwe kuondoka maeneo ya ufukweni ili kujihami.
Francis Mossongo,
Afisa mwandamizi Ubalozi wa Tanzania,Tokyo...12, March, 2011
Wakati huo huo... ++ Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika Vilivyoitaarifu Mirindimo hivi punde watanzania wote wako salama hapa Japani...
Watu 650 wamethibitika kufariki dunia kote Japani kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea jana jioni majira ya saa 9 kasorobo. Hadi narejea nyumbani jana usikuu,(saa 6:56) kwa saa za hapa, usafiri umevurugika, na mitandao ilipata kwikwi..Lilianza tetemeko la kishindo na kuishia na mawimbi hatimaye vifo.
Tetemeko hilo kubwa lenye ukubwa wa 8.9 kipimo cha richa limetikisa maeneo mengi ya Japani na kudumu kwa dakika kadhaa.Mbali na vifo 650, wengi hawajulikani walipo achilia mbali walio na majeraha.Polisi wameitaja namba hiyo ya vifo wakisema kuwa huenda ikaongezeka lakini hadi kufikia wakati huu naandika ripoti hii duru rasmi zimesema kuwa vifo vilivyothibitishwa ni 185, watu 741 wamepotea na 948 wamejeruhiwa. Kupotea huku kunaashiria habari za vifo kuwezeza kupkelewa tena na tena.
Hali ya taharuki ilionekana waziwazi katikati ya jiji la Tokyo ambapo watu walionekana kukimbilia maeneo ya wazi na yale yaliyotengwa maalum watu kwenda yanapotokea maafa. Waliokuwa ofisini walikimbili chini ya viti, wengine wakipiga magoti kuendesha ibada za kimya kimya na wengine wakikimbia kutoka katika ofisi zao hasa zilizopo magorofani.
Majengo mengi yalinusurika kuanguka au kuwaka moto kutokana na teknolojia iliyotumika na hivyo kuyafanya yanese. Hata hivyo katika maeneo ya Pwani kaskazini ya Japani ambako kingo za maji zilikuwa chini ya mita saba maji yaliparamia kuta na kuingia katika majumba ya watu.
Shirika la Utabiri wa hali ya hewa baada ye lilisema kuwa kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa kilometa 400 kutoka Tokyo , kilometa 20 chini ya ardhi .Limetoa hadhari kuwa huenda yakazuka mawimbi makubwa ya tsunami yanayofikia kimo cha mita sita hadi kumi katika pwani ya mkoa wa Miyagi. Na inaripotiwa kuwa mawimbi ya kimo cha mita kmi yalipiga muda mfupi tu baada ya tetemeko huko Miyagi.
Televisheni ya Shirika la utangazaji la Japani –NHK zimeonyesha mawimbi ya tsunami yakisomba magari katika eneo la Miyagi na kiwanda cha kusafisha mafuta kilichopo katika jiji la Ichihara katika mkoa wa Chiba kiliripuka na kuleta hali ya taharuki kubwa. Haijulikana kama kuna mtu amekufa ama kujeruhiwa.
Katika jengo la utangazaji la NHK wandishi wa habari waliendelea na wajibu wao ,kujua kinachoendelea kila kona ya Japani huku wakiwa katika hali ya taharuki na kituo chake cha televisheni kiliendelea kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka mikoa mbalimbali ya hapa Japani, na waandishi wake kujitosa katikati ya hali inayotisha kupata picha ya kile kinachoendelea..
Vituo vya habari vya NHK –Japani, BBC, na CNN viliendelea na matangazo ya mara kwa mara yakionyesha mawimbi makubwa yalionekana yakisomba vifusi, nyumba , kubomoa madaraja na magari yalikuwepo karibu na fukwe za bahari.
Huko jiji la Miyagi Barabara kuu zimeharibika. Huduma treni ziendazo kasi na zile za kawaida zilisimama nchi nzima huku wataalamu wakipita huku na kule wakiwa katika makundi, wale wanaotafuta waathirika , kuangalia miundo mbinu kama vile reli na barabara na madaraja kama vinaweza kutumika bila madhara na mitandao ya intaneti.
Inakadiriwa kuwa hadi sasa kuwa kaya millioni 4 zimeathirika kwa njia moja ama nyingine katika jiji la Tokyo. Itakumbukwa kuwa jana alhamisi tetemeko lenye ukubwa wa 6.3 kipimo cha richa lilipiga eneo la Honshu na mtetemo wake kusikika jijini Tokyo. La leo limefikia 8.9 na kumbukumbu inaonyesha kuwa tetemeko lililovunja rekodi kwa ukubwa duniani hadi sasa ni lile la mwaka 1960 lililotokea nchini Chile mwaka 1960 tarehe 22 , may ambalo lilifikia ukubwa wa 9.5 kipimo cha richa . Pengine tofauti na matukio kama haya ya miaka ya karibuni tetemeko la leo limedumu kwa muda mrefu na limeuwa likijirudia na mara ya mwisho ilikuwa saa 12 kasoro jioni jioni saa za huku ambako Afrika Mashariki ni saa 6 kasorobo.(CNN)
Mwandishi wa BBC aliyopo Tokyo , Roland Buerk anasema kuwa watu wengi huenda wamejeruhiwa na tetemeko hili na kwamba tetemeko la aina hii halijawahi kutoka katika kipindi kirefu kilichopita. Hadhari ya kutokea kwa mawimbi makubwa ya tsunami imetolewa kuwa huenda nchi nyingine kadhaa zitaingia kwenye hali ya wasiwasi ikiwa ni pamoja Ufilipino, Indonesia, Taiwan, na pwani ya Pasifiki nchini Urussi pamoja nna Hawaii.
Habari za hivi karibuni zinasema kuwa watu wengine 20 wamekufa baada ya kuangukiwa na paa walipokuwa katika hafla ya kumaliza masomo katikati ya jiji la Tokyo. Na huko Fukushima kuna habari ya vifo. Idadi itajulikana baadaye…Viwanja wa ndege vya Narita na Haneda vilifungwa kwa muda lakini sasa vimefunguliwa upya , na vinu vya nyuklia kwa ajili ya nishati vilijizima vyenyewe na kuondoa wasiwasi wa kuvuja na ufuatiliaji unaendelea. Waziri Mkuu Naoto Kan aliwaambia wananchi wa Japani wawe wastahimilivu na kwamba vinu vya nyuklia viko salama.
Wakati huu Shirika la Utangazaji la japani linaendelea kutoa matangazo ya moja kwa moja juu ya maafa haya ...na taarifa nyingine nitawapa baadaye...na hasa idadi ya vifo na athari nyingine...Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania hapa Japani Mh. Salome Sijaona ambaye aliongea na NHK , hakuna taarifa za kupotea kwa maisha kwa mtanzania yoyote ingawa , mmoja wa watanzania anayeishi karibu na maeneo yaliyopata athar kubwa hajafanya mawasiliano yoyote na wengine na bado anafuatiliwa kujua kulikoni. Unaweza kusikiliza mahojiano hayo kwa kubofya hapo kulia -Mtandao Rafiki NHK World Swahili, then nenda kwenye habari na pia hakuna mwana-Afrika Mashariki aliyethibitika kufa na zikipatikana habari hizo tutawajulisha.