Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, December 14, 2009

Kunako chombo...speed boat . Paparazi wa Kimataifa Peter Omari akiwa katika majukumu ya kukusanya habari huko Zanzibar Leo J3 mchana. Fuatilia taarifa kwa njia ya picha. Mgosi usikose kuonja mishikaki ya forodhani, na shurti ule miwili. Unguja raha anayetaka na aje! eeh tunakaribia...
Vo hapo bandarini Ungujaa! Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja zanzibar...
Usafiri hapo Forodhani waelekea kwetu Bwejuuu! Bwawani hoteli muonekano wa leo mchana...
Mitaa ya mji Mkongwe ...eneo hili ni uriyhi wa dunia unaotambuliwa na Umoja wa Mataifa. Ngome Kuu ndani ya mji Mkongwe -Unguja

Posted by BM. on Sunday, December 13, 2009


Moja ya vikorombwezo vya jiji la Mwanza , ukiona picha hiyo tu unaweza kusweka matonge bila shida. Hongereni kwa ubunifu; wale walobuni hii!
Hapa jana jijini Mwanza palikuwa hapatoshi, Chuo cha Biashara CBE , kulikuwa na mahafali na watu walipata nondos zao, Hongereni sana .Walo mbali na wa karibuni fuatilieni tukio hilo kwa njia ya picha. Mgeni rasmi katika mahafali hayo ,Naibu waziri wa biashara na masoko Mh. Cyril Chami akiwahutubia wahitimu na waalikwa. Baadhi ya wahitimu wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kupewa vyeti vyao. MC alikuwa mtangazaji wa siku nyingi wa Star TV na Redio Free Africa, Bi. Joan Itanisa ambaye sasa ni mhadhiri msaidizi St. Augustine University. Take 5 Mc, tumekubali.
Brass Band kutoka makutupora JKT ilikuwepo. Inanikumbusha zile enzi za ....Wee kurta!
Kikundi cha Utamaduni cha wasukuma wa Bujora na ngoma ya nyoka. Du inataka moyo!
Bila huyu ....Msukuma hajaanua ngoma; wejemeni!

Posted by BM. on Friday, December 11, 2009

Safari ya mwandishi wa habari Peter Omari wilayani Kibondo; ili kuhakikisha usalama wake ulinz ni jambo muhimu. Njia moja... Mgosi Peter Omari akiwa katika msafara kuelekea Kibondo chini ya Ulinzi maana jmaa hawachelewi.
Ndio Maana yake Daraja la mto Malagalasi linalotenganisha wilaya za Kasulu na Kibondo.
Maktaba ya shule ya wasichana Mkugwa wilayani Kibondo iliyojengwa kwa msaada wa UN Mto Malagalasi unavyoonekana kutoka angani!

Posted by BM. on Friday, December 11, 2009


Mkoa wa Shinyanga na mandhali yake ya kiasili.

Posted by BM. on Friday, December 11, 2009

Raisi Jakaya Kikwete amemteua Mh.Salome Sijaona kuwa Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Japani hivyo kuchukua nafasi ya Mh. Elly Mtango ambaye amestaafu. Kabla ya uteuzi huo Mh. Sijaona alikuwa Katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi na maendeleo ya makazi. Picha ya Juu Mh. Sijaona kwenye komputa.

Posted by BM. on Thursday, December 10, 2009

Kama wewe ni mpenzi wa Bakulutu ya taratibu Msikilize mwanadada huyu aayeibukia huko DRC Diva Barbara Kanam ...Cheri Mpenzi uone wenzetu wnavyojitahidi kufikisha ujumbe katika Lugha Ngeni. Nimependa kompozisheni yake halafu nenda kwa Koffi Antonio Olomide hapo chini. Hii ni kiondoa maumivu.
Haya unasemaje!

Posted by BM. on Thursday, December 10, 2009

No Comment.

Posted by BM. on Thursday, December 10, 2009


Heshima kutoka kwenye vikosi vya Majeshi kwa Mkuu wa nchi.
Ukakamavu....

Raisi Jakaya Kikwete akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali David Mwamunyange katika maadhimishoya Sherehe za Uhuru miaka 48 jana jijini Dar.(Picha zote na Ikulu)

Posted by BM. on Thursday, December 10, 2009

Njia ya kuelekea Kijijini kwetu...kaskazini mashariki ya Kenya Mvua zimepiga sana.

Teknolojia hii unaionaje...nadhani itapunguza ajali ukitaa kwenda kulia unawasha indiketa...du hii nayo!
Rasilimali mwili!
Matumizi mbadala ya rasilimali...!

Posted by BM. on Saturday, December 05, 2009


Muda mfupi uliopita usiku huu wa Jumamosi hafla imekwisha katika Chuo Kikuu cha Soka hapa Japani, ambapokulifanyika mashindano ya 19 ya hotuba kwa lugha ya Kiswahili ya kuwania kombe la mwasisi wa Chuo kikuu cha Soka Bw. Daisaku Ikeda. Pitia Picha hicho ili upate picha ya kile kilichotokea leo....Hapo ni jumba moja ya Chuo hicho ambacho huifadhi nyaraka na medali mbali ambazo chuo hicho imepata katika hafla mbalimbali...

Timu nzima ya waalikwa kwenye mashindano hayo. Kushoto mwongozaji wetu Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Mr. Francis Musongo , Bm , Mwakilishi wa Balozi wa DRC hapa JP Mulumba Tshindimba Mr. Mwenda na Bi Grace wa Ubalozi wa Tz hapa JPna mwongozi wetu mwingine. Pozi la chapchap!

Nami nilipata kuzungumza kama mmoja wa majaji.. Burudani nayo ilikuwepo...

Da Mariamu akiwa na mshindi... Hawa ndio Ma Mc wa shughuli yaleo hapa Soka university..wamefanya kazi nzuri sana.
Picha ya pamoja; Grace, mshindi wa kwanza Bi.Masako Kitaura,Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania Japani Fancis Mussongo Da Mariam, Bw. Mwombeki , Kiongozi wetu mwandamizi wa Jumuia ya watanzania wanaoishi Japani ,BM.

Mmoja wa Viongozi waandamizi wa TANZANITE -JP Mr. Mwombeki (Kulia)alikuwepo.

Watanzania walifika kutoa support ya kukuzwa kwa Kiswahili....

Posted by BM. on Friday, December 04, 2009

Fuatilia nyimbo zake..

Posted by BM. on Friday, December 04, 2009


Peter Omari , Paparazi wa kimataifa anaendelea na jukumu maalum nchini Tanzania la kuandaa Radio Documentary inayoitwa ONE UN lengo likiwa kuonyesha mafanikio ya mashirika ya umoja wa mataifa pale yanapofanya kazi kwa pamoja (One UN) kwa kujiratibu vizuri zaidi.Tanzania ni moja ya nchi nane duniani zinazo tekeleza mpango wa pamoja wa umoja wa mataifa kwa majaribio. Nchi nyingine ni Albania, Msumbiji, Pakistan, Rwanda, Uruguay, Vietnam na visiwa vya Cape Verde. Kwa Tanzania mpango huo wa Umoja wa mataifa umeanzisha programu mbalimbali za pamoja zikikusudia pamoja na mambo mengine kuchangia kutekelezwa kwa mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Tanzania (MKUKUTA na MKUZA kwa Zanzibar) na pia kufanikisha kufikiwa kwa malengo ya maendeleo ya Milenia. Itl.P.P.O kwa sasa ni Meneja wa Kiss FM ya Mwanza chini ya Sahara Communication Ltd.Fuatilia kazi zake kwa njia ya Picha.
Mpanda International airport..Rukwa.
Watoto hawa walio na ulemavu wa ngozi wakiwa katika kambi ya Kabanga huko Kasulu wanalindwa na mitutu ya Bunduki kuokoa maisha yao ...Inasikitisha sana na haiingii akilini ukifikiria kuwa hiyo ndio Tanzania ya karne ya 21 Kaburi la aliyekuwa Paparazi wa kutumainiwa huko Kasulu... Kwa kifupi Deogratius Kiduduye alifariki dunia Mwezi May mwaka huu kwa ugonjwa wa kisukari kwa mujibu wa matangazo yaliyotolewa na Radio Free Afrika,Mwanza ambako alikuwa miongoni mwa watangazaji wa kwanza walioanzisha redio hiyo hapaTanzania .Mpaka mauti yanamkuta Kiduduye alikuwa ni mtangazaji katika kituo cha Radio Uhuru cha jijini Dar es salaam. Ana kila sababu ya kukumbukwa.
Enzi ya uhai wake Marehemu Kiduduye picha ya Juu (KUSHOTO) akiwa Lusaka Zambia. Picha kwa hisani ya Mtangazaji Blog. Peter Omari alifika kwa mama yake Kiduduye kuhani. Picha ya Kumbukumbu.

Ukiona kibao umefika! Mdau mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wanavijiji wanaoishi jirani na kambi ya wakimbizi ya Viyowesi -Kasulu
Katika Majukumu;Afisa Mipango wa wilaya ya Kasulu Bw. Bwire Mjuberi akiongea na Int.PP.O