Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, December 11, 2010

Fresh Jumbe Mkuu sio tu mwanamuziki lakini 'mhadhiri' kupitia fani yake.... . Nina hamu sana usikilize muziki huu , huku ukisiliza hoja zake..nakukubali Fresh. Kesho Dec, 12 ataporomosha muziki wake katika jiji la Sagamihara hapa Japani mbele ya watanzania wenzake na wageni wengine katika kuadhimisha miaka 49 ya uhuru wa tanzania bara...! Tutajumuika na tutakujuza!

Posted by BM. on Saturday, December 11, 2010

Darasa ;

Posted by BM. on Saturday, December 11, 2010

Kalamu ya paparazi inapoonwa na Mkuu wa nchi.

Posted by BM. on Monday, December 06, 2010

Hii ina nikumbusha Ivory coast. Mungu apishilie mbali yasitokee kama ya Kenya .
Huko Ivory Coast tunaelezwa kuwa ...Tayari Raisi wa zamani wa Afrika Kusini na mwakilisi wa AU Thabo Mbeki, amekwishakutana na wagombea wawili wa rais wa Ivory Coast ambao walijitangaza kuwa rais wa nchi hiyo mjini Abidjan hapo siku ya Jumapili ilikutafuta suluhisho la mgogoro huo.Bw. Mbeki aliwambia waandishi habari kwamba amekwenda huko kusikiliza kila upande ili kufahamu jinisi hali ilivyo lakini Bw. Outtara amewambia waandishi habari kwamba alimuarifu Bw. beki kwamba yeye ndiye rais wa halali wa nchi na amemtaka Bw. Gbagbo kumkabidhi madaraka.



Laurent Gbagbo alikula kiapo ya kuiongoza nchi siku ya Jumamosi kwa misingi kuwa, baraza la katiba limempa ushindi wa asilimia 51 ya kura. Takriban asilimia kumi ya kura zilibatilishwa kwasababu ya ubadhirifu.
Madai ya Bw. Ouattara ya kushinda uchaguzi yanaungwa mkono na Jumuia ya Kimataifa.
Hakuna dalili ya kumalizika kwa mzozo huu kwa urahisi labda kwa kugawana madaraka , fomula iliyo nyepesi pindi maamuzi ndani ya masanduku ya kura yanapochafuliwa .

Posted by BM. on Sunday, December 05, 2010

Wagombea wote wa nafasi ya Uraisi nchini Ivory Coast ambao walipambana katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini humo wameamua kujiapisha kila mtu kivyake na hivyo kuwa na nchi yenye 'Maraisi wawili' wakati huu , hali inayolikaribisha taifa hilo kwenye vita na machafuko makubwa.

Rais anayetetea kiti chake Laurent Gbagbo(anayeapa hapo chini) alikuwa wa kwanza kujiapisha na saa chache baadaye mwenzake naye Alassane Ouattara pia akala kiapo kuliongoza taifa hilo kwa uaminifu mkubwa na kwa maana hiyo kuwa nchi ya kwanza duniani katika historia kuwa na maraisi wawali na kwa maana hiyo Maamiri majeshi wakuu wawili...imagine!.

Marekani, Umoja wa Mataifa na Ufaransa zimesema Bw Ouattara ndiye ameshinda uchaguzi huo.Bw Ouattara alitangazwa mshindi la Tume ya Uchaguzi, lakini matokeo hayo yalitenguliwa na Baraza la Katiba, ambalo linaongozwa na mshirika wa Bw Gbagbo.
Uchaguzi wa raundi ya pili ya urais, ulikuwa na lengo la kuliunganisha taifa hilo ambalo ndio mzalishaji mkubwa zaidi ya kakao duniani, baada ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.
Maelfu ya wakazi wa nchi hiyo waliingia mitaani kwa maandamano wakipinga hatua ya Bw Gbagbo, wakisema hayo ni mapinduzi. Huku wafuasi wa Gbagbo wakiangusha kicheko kilichojaa wasiwasi. Inavyooelekea Allassane Ouattara anaungwa mkono na watu wengi nchini humo kuliko mwenzake...unaweza kuangalia sehemu ya kampeni zake...
Wafuasi hao wa Bw Gbagbo wanasisitiza kuwa Umoja wa Mataifa hauna haki ya kusema nani ni mshindi, na wametishia kuwafukuza wafanyakazi wapataoo 8,000 wa umoja huo. Sijui ! lakini sakata hili haliwezi kwisha hvi hivi bila ghasia na pengine vifo...

Posted by BM. on Saturday, December 04, 2010

Posted by BM. on Saturday, December 04, 2010

Inatajwa kuwa aina hiyo ya pilipili ni kali kuliko zote duniani. Inapatikana Mexico..Inasemekana imetokana na mchanganyiko wa aina kadhaa za pilipili zilichanganywa kwenye maabara za mbegu katika Chuo Kikuu cha Warwick.

Kuna jamaa mmoja anaitwa Fowler anasema ukila tu kwanza unasikia maumivu ya ladha chungu halafu uuuuwiii... unaanza kuwashwa. Jamaa anasema ukiila lazima unyamaze kimya kwa muda wa dakika kadhaa kichozi kikutoke then Ghuuu...! ..du!

Posted by BM. on Saturday, December 04, 2010

Hospitali kubwa ya kwetu...soma bango...

Posted by BM. on Saturday, December 04, 2010


Bro Khalifa katika pozzz huko Kusini mwa Afrika...5

Posted by BM. on Saturday, December 04, 2010

Uchovu hauna Makomandoo; wanajeshi wa Marekani wakiwa Kandahar baada ya mikiki mikiki mingine usngizi unafuata...

Posted by BM. on Thursday, December 02, 2010

Mchana wa leo wakati wa mlo nilitoka katika jengo la iutangazaji la shirika la Utangazaji la Japani geti la Mashariki nikaelekea kaskazini ambako kuna bustani nzuri ya Yoyogi. Hapo nikakutana na makundi ya watu wakipiga picha. Nilipoongea nao wakasema wanashinda hapo kila siku kutafuta picha nzuri za ndehge na wanyama wadogo watambaao eeh! Ni hobi yangu kupiga picha na hivyo nikafurahi kukutana na wadau. Ambatana nami...









Aina ya ndege zinazosakwa na kamera ni hizi...


Kuna sanamu pia bustanini ambayo watu hupenda kuipiga picha ,nami pia nikaifyatua...


Nami nikafyatuliwa...pwaa!

Posted by BM. on Wednesday, December 01, 2010

Nimefuatilia kwa makini simulizi hii ya waandishi wa habari wa Kenya nimeridhika kuwa wamefanya kile tunachokiita chunguni kama 'Habari za uchunguzi' . wanaopenda kazi ya uanahabari na wanahabari wenyewe wanaweza kufuatilia taarifa hii na kisha tuchangie maoni yetu.

Hongereni jicho pevu...nimewakubali....

Posted by BM. on Wednesday, December 01, 2010

Ukipenda tabasamu!

Posted by BM. on Tuesday, November 30, 2010


Kwa hisani kubwa ya NTV-Kenya..

Posted by BM. on Tuesday, November 30, 2010

Tetemeko lenye ukubwa wa 6.9 kwa kipimo cha richa limetikisa pwani ya kusini ya jiji la Tokyo nasi katika jengo la utangazaji limetutikisa kwa muda wakati tukiendelea kurusha matangazo.Majengo yalitikiswa katikati ya Tokyo lakini kutokana na kuwepo kwa teknolojia ilionekana kama vile yakiyumba hivi.

Hakuna majeruhi wala uharibifu ulioripotiwa hadi sasa na idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa hakuna tisho la kuwepo kwa mawimbi ya tsunami kwahiyo hali inatarajiwa kuwa shwari.Mtetemo huo ulitokea saa sita na dakika 25 mchana huku kitovu cha tetemeko hicho kikitajwa kuwa kilikuwa karibu na visiwa vya Ogasawara takriban kilometa 800 na lilitokea kilometa 480 chini ya ardhi . Ingawa vipimo vya idara ya hali ya hewa ya Japani inasema kuwa tetemeko lilikuwa na ukubwa wa 6.9 , ile ya Marekani ilisema ilikuwa na ukubwa wa 6.6.