Ni hapa...
duh ...Hakuna kuchelewa...au siyo!
Jana tulirekodi kipindi chetu cha 'Sauti ya Antyango' Katika Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani hapa Tokyo nikiwa na mtayarishaji mwenzangu msanii maarufu wa ngoma za kijadi za Afrika Mashariki hususan Kenya ya Nyatiti Bi. Erico Mukoyama maarufu Anyango! ambapo tuliwachambua wanamuziki kadhaa akiwemo Sakaki Mango, huyu anacheza chombo cha asili cha kigogo cha limba...
Baadaye nilifanya mazungumzo na mdada wa Kifaransa..Bi Amina Abdala...yeye ni mzaliwa wa Lamu kule Kenya lakini amekulia Ufaransa na sasa ni director wa Anyango Foundation huko Ufaransa , ambayo inaratibu ziara za Anyango barani Ulaya , kufundisha muziki wa kijadi huko pamoja na kusambaza CDs.
Recording hiyo ilishuhudiwa na Mkuu wa Idhaa za Kigeni wa NHK , Bi, yuko Asano na wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili...
Amina alipata fursa ya kunionyesha kazi anazofanya huko Ufaransa alizozihifadh kwenye komputa yake,...
Ukipenda kumuona Mjapani anayecheza ngoma za Kigogo Sakaki Mango bofya hapo chini.....
Kwenye mtandao mmoja wa Kibiashara, bidhaa mbili mpya zimetangazwa. Moja ni Mo na nyingine aina mpya ya gari ya Mazda. Nakuletea picha zake...
Mo:Ben ni chombo kidogo cha nyumbani ambacho kimejengewa kikanza (Heater) ambacho kinaweza kupasha moto chakula na kuurejesha ujoto uliokuwepo awali. Ni kiasi cha ku-tyuni tu joto linaanza kusambaa kunako kikanza. Vifaa vya namna hii viko vingi Japani lakini kinachofanyika ni kuvipa muundo mpya kila kukicha..
Aina mpya ya gari ‘Mazda’ imejitokeza kuingia kwa vishindo katika soko la magari ya kifahari nchini Japani na kufahamika sana kwa jina la “Kiyora”. Kwa kijapani Kiyora ina maanisha ‘Safi na halisi’ ikiwa na silinda nne , injini inayotoa kiwango kidogo cha kaboni na inatumia mafuta machache. Umbile lake ni la kipekee na linavutia. Unaweza kumuona dereva akiwa ndani ya gari na maji ynayotiririka kuleta ubaridi katika gari…
Hivi karibuni , mbao za matangazo katika Chuo Kikuu Cha kilimo cha Tokyo maarufu kama Tokyo NODAI hapa Japani zilikuwa zimepambwa kwa matangazo kama inavyoonekana hapo pichani.
Matangazo hayo yaliyokuwa yameandikwa kwa Kijapani na picha nzuri za wanyamapori, na bendera ya Tanzania yalitumika kuwaalika watu kuja kujumuika katika Tafrija ya kubadilishana utamaduni wa Chakula (Food Culture Exchange Party) au kwa lugha rahisi hujulikana kama 食文化 パーティ. (Mdau Eustadius Francis akiwa katika harakati..... )
Hii ilikuwa mara ya kwanza kabisa kwa nchi ya Afrika kushiriki kwenye tafrija hizi. Katika tafrija hiyo wanafunzi wajapani wengine kutoka nchi mbali mbali wanaosoma chuoni hapa walishiriki. Kabla ya mapishi kuanza kulikuwa na presentation inayoelezea Tanzania kwa Ujumla.
Kwa hiyo siku hiyo Wajapani walielekezwa namna ya kupika wali wa nazi, mchuzi wa kuku ulioungwa kwa nazi pamoja viungo vingine. Pia tuliwaekeza namna ya kutengeneza Kachumbari ya nyanya, karoti, tango, vitunguu maji na limao. Baada ya maelekezo, kila kundi lilijiweka sawa na kutengeneza msosi bomba kabisa wenye asili ya pwani.
Hali iliyomfanya kila Mtanzania aliyekuwepo hapo kujihisi yupo nyumbani. Baada ya tafrija, waandaji waliahidi kuwa siku nyingine watapiga ugali.
Jitihada za kupata unga kutoka makampuni ya nyumbani tanzania zinaendelea ili ugali uweze kutinga katika Mesi za Chuo hicho hivi karibuni. Thanx mdau Eustadius Francis ...
Polisi nchini Japani imemfungulia mashitaka binti mmoja wa kijapani kwa kitendo chake cha kuongea na simu ya mkononi wakati akiendesha baiskeli. Hii ni kesi ya aina yake hapa nchini kutokana na ukweli kuwa japo kuna sheria inayokataza kitendo hicho lakini ni mara chache kesi hizo kujitokeza mahakamani. Saa tatu ya jumapili iliyopita , Polisi aliyekuwa akifanya doria huko Hiratsuka, katika mkoa wa Kanagawa , alimuona binti mmoja mwanafunzi wa sekondari mwenye miaka 15 akiwa anazungumza na simu akiwa anaendesha baiskeli na kwa maana hiyo kuvunja sheria ya barabarani na mbaya zaidi alipoambiwa aache kufanya hivyo alikaidi.
Mwanafunzi huyo alijikuta akiandikiwa hati ya kufikishwa mahakamani , ikiwa ni mara ya kwanza kwa polisi wa eneo hilo la kufikisha mahakamani shauri linalofanana na hilo , wakidai kuwa wanataka kukomesha vitendo vinavyofanywa na waendesha baiskeli hapa Japani vya kuongea na simu wakati wakiendesha baiskeli au kusikiliza muziki kwa kutumia vifaa vidogo vya muziki masikioni huku wakiwa katika mwendo mkali katika baiskeli zao.. Sheria inayokaza vitendo hivyo ilianza kutumika rasmi tarehe mosi mwezi Mei mwaka huu.Bila shaka binti huyo akipatikana na hatia atapigwa faini ya Yeni za kijapani elfu 50 sawa na fedha za kitanzania Takriban (Tsh. 975,000/=)
Nasi mashabiki wa baiskeli inabidi tuwe makini ...duh!-